OFA £ 40,000,001: SUAREZ RUKSA KUONGEA - TopicsExpress



          

OFA £ 40,000,001: SUAREZ RUKSA KUONGEA NA ARSENAL…….!! Wednesday, 24 July 2013 21:15 >>MMLIKI LIVERPOOL AHOJI: ‘EMIRATES WANAVUTA NINI?? ’ >>HIGUAIN, REINA WATUA NAPOLI!! LUIS SUAREZ yuko huru kuzungumza na Arsenal lakini hataruhusiwa kuihama Liverpool hadi pale thamani yake ya Pauni Milioni 50 na ushei itakapofikiwa na huko Italy, Klabu ya Serie A Napoli leo imewapokea Gonzalo Higuain na Pepe Reina kwa ajili ya upimwaji afya kabla hawajakamilisha Uhamisho wao. Luis Suarez: Arsenal ruksa kuongea nae! LUIS SUAREZ yuko huru kuzungumza na Arsenal lakini hataruhusiwa kuihama Liverpool hadi pale thamani yake ya Pauni Milioni 50 na ushei itakapofikiwa. Hapo Jana Arsenal ilitoa Ofa ya Pauni 40,000,001 ambayo ilikataliwa na Liverpool. Ofa hii, yenye idadi ya Fedha ya ajabu kidogo, ni ya makusudi ili ‘kuamsha’ Kipengele cha Mkataba wa Suarez ambacho kinaitaka Liverpool kutafakari Ofa yeyote ya kumnunua Suarez itakayotolewa ikiwa tu imevuka Pauni Milioni 40 na pia ni wajibu Mchezaji huyo kujulishwa kuhusu Ofa hiyo na pia kuruhusiwa kuongea na huyo mtoa Ofa. Lakini, Kisheria, Liverpool hawawajibiki kumuuza na hivyo ndivyo walivyofanya kwa kuikataa Ofa hii ya sasa ya Arsenal. Sasa Suarez, ambae leo ameichezea Liverpool huko Australia ikiwa ni Mechi yake ya kwanza tangu amng’ate Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic kwenye Mechi Mwezi Aprili, ameiambia Liverpool kuwa atazungumza na Arsenal. ++++++++++++++++++++++++++ ++++ ARSENAL==BEI MBAYA KUNUNUA WACHEZAJI: -Jose Antonio Reyes (Sevilla) Pauni Milioni 17.5 -Santi Cazorla (Malaga) Pauni Milioni 16 -Andrey Arshavin (Zenit St Petersburg) Pauni Milioni 15 -Sylvain Wiltord (Bordeaux) Pauni Milioni 13 -Thierry Henry (Juventus) Pauni Milioni 11 ++++++++++++++++++++++++++ ++++ Hadi sasa, Liverpool wameshazikataa Ofa mbili kutoka kwa Arsenal za kumnunua Suarez ambae pia anadaiwa kutakiwa na Real Madrid ambao, hata hivyo, hawajatoa Ofa rasmi. Mara baada ya Arsenal kutoa hii Ofa ya ajabu, Mmiliki wa Liverpool, John W. Henry, ambae ni Raia wa Marekani, aliibukia kwenye Ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter na kuposti: “Unafikiri wanavuta nini huko Emirates?” Hata hivyo, posti hii haikueleweka ina maana gani hasa ama juu ya Arsenal kumtaka Suarez au thamani yake Suarez. Wiki iliyopita Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, alisema thamani halisi ya Luis Suarez ni sawa na Edinson Cavani ambae hivi karibuni alijiunga na Paris St-Germain kwa Dau la Pauni Milioni 55. Higuain & Reina watua Napoli Gonzalo Higuaín na Pepe Reina wamewasili Nchini Italy ili kupimwa afya zao Klabuni Napoli tayari kwa ajili ya kukamilisha Uhamisho wao. Higuain, Straika kutoka Argentina mwenye Miaka 25, anatarajiwa kuhamia Napoli kutoka Real Madrid kwa Dau la Pauni 34.5 na atapewa Mkataba wa Miaka mitano. Nae Kipa wa Liverpool ambae pia ni Kipa wa Spain, Pepe Reina, anaungana tena na Meneja Rafael Benitez baada ya kutua Napoli kwa Mkopo wa Msimu mmoja. Reina amelazimika kukimbilia Napoli baada ya Liverpool kumsaini Kipa wa Sunderland, Simon Mignolet, ambae ndie anakuwa Nambari Wani. Higuain amekuwa pia akihusishwa na Klabu ya England Arsenal lakini sasa hapo Napoli anaungana na wenzake wawili waliotoka Real Madrid kipindi hiki, José Callejón na Raul Albiol. Mchezaji mwingine mpya alienunuliwa na Meneja mpya Rafael Benitez ni Dries Mertens toka PSV Eindhoven.
Posted on: Wed, 24 Jul 2013 19:03:42 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015