Orodha ya majiji kumi yanayoongoza kuwa na ma ‘$ milionea’ - TopicsExpress



          

Orodha ya majiji kumi yanayoongoza kuwa na ma ‘$ milionea’ wengi zaidi Afrika, Tanzania haimo! August21,2013 Johannesburg mji mkuu wa kibiashara wa Afrika Kusini, ndio jiji linaloshika nafasi ya kwanza katika orodha ya majiji kumi yenye watu matajiri wengi zaidi Afrika ‘dollar Millionaires’. Johannesburg Ripoti hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na New World Wealth ya Oxford, Uingereza. Johannesburg jiji linalofahamika pia kama ‘city of gold’ imeongoza orodha hiyo kwa kuwa na idadi ya matajiri wasiopungua 23,400 , ikifuatiwa na jiji la Cairo, Misri lenye matajiri 12,300. Jiji la tatu katika orodha hiyo ya majiji yenye mamilionea wengi zaidi Afrika ni Lagos, Nigeria yenye idadi ya 9800. Lagos Afrika Kusini imefanikiwa kuingiza majiji manne katika orodha hiyo, mengine yakiwa ni Cape Town iliyokamata nafasi ya nne kwa idadi ya 9000, Durban katika nafasi ya tisa ikiwa na 2700, na Pretoria nafasi ya 8 ikiwa na matajiri 2500. Nchi pekee ya Afrika mashariki iliyoingia katika orodha hiyo ni Kenya, ambapo jiji la Nairobi likiwa na ‘dollar Millionaires’ 5000 na kukamata nafasi ya tano, huku Uganda na Tanzania zikiwa hazijaingia kabisa katika orodha hiyo. Nairobi Miji mingine ni Casablanca, Morocco katika nafasi ya saba ikiwa na 2700, mji wenye gharama kubwa za kuishi Luanda, Angola katika nafasi ya tisa ikiwa na 2400, huku orodha hiyo ikifungwa na Algiers , Algeria kwa kushika nafasi ya kumi kwa kuwa na matajiri 2300. Katika Top 10 ya nchi, Afrika Kusini ndiyo inakamata nafasi ya kwanza kwa kuwa na mamillionea 48,800 ikifuatiwa na Misri 23,000 na nafasi ya tatu ni Nigeria kwa 15,900. Kwa mujibu wa New World Wealth, “Millionaire” inamaanisha watu binafsi wenye mali za kuanzia $1m na kuendelea, ukiondoa makazi yao. Hii ndio orodha kamili ya majiji kumi yanayoongoza Afrika 1. Johannesburg, South Africa – 23, 400 2. Cairo, Egypt – 12, 300 3. Lagos, Nigeria – 9, 800 4. Cape Town, South Africa – 9, 000 5. Nairobi, Kenya – 5, 000 6. Durban, South Africa – 2, 700 7. Casablanca, Morocco – 2, 700 8. Pretoria, South Africa – 2, 500 9. Luanda, Angola – 2, 400 10. Algiers, Algeria – 2, 300 Source: vorbe margzn, the gurdian
Posted on: Wed, 21 Aug 2013 14:48:14 +0000

Trending Topics




© 2015