Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela anasalia - TopicsExpress



          

Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela anasalia hospitalini kwa siku ya tatu baada ya kupata maradhi ya mapafu kwa mara nyingine tena huku serikali ikionekana kuwa kimya kuhusu hali ya shujaa huyo Familia yake ilionekana hapo jana ikitoka katika hospitali moja mjini Pretoria.Hii ni mara ya nne kwa Mandela kulazwa hospitalini tangu mwezi Desemba mwaka jana.Akizungumzia hali yake msemaji wake Mac Maharaj amesema kiongozi huyo anapumua bila usaidizi lakini akasema hali yake si nzuri. Raia wengi wa Afrika kusini hapo jana walikusanyika makanisani kumuombea Mandela mwenye umri wa miaka 94.Lakini wengi wa raia hao wanaanza kukubali kuwa hata yeye shujaa wao rais wa kwanza mweusi nchini humo ni mwanadamu na lolote laweza mfika. Gazeti la Sunday Times hapo jana lilikuwa na kichwa cha habari kilicho onyeesha ukweli wa mambo kuwa ni wakati wa kumuacha aende.Rafiki yake wa muda mrefu Andrew Mlangeni mwenye umri wa miaka 87 aliliambia gazeti hilo kuwa wanamtakia Madiba afueni ya haraka lakini anadhani la muhimu ni kwa familia yake kukubali na kumruhusu akapumzike. Mandela augua Mandela augua Mlangani ambaye walifungwa na Mandela jela mwaka 1964 ameongeza kuwa punde familia yake ikikubali hilo, watu wa Afrika kusini pia watafuata mkondo na kutoa shukran kwa Mungu kwa kuwapa mtu huyo maishani mwao. Shujaa wa Afrika alemewa na maradhi Mandela ambaye anafikisha miaka 95 mwezi ujao anaenziwa si Afrika kusini tu bali bara zima la Afrika na ulimwengu kwa jumla kama kielelezo cha amani na maridhiano kufuatia kuachiliwa kwake kutoka jela alikozuiliwa kwa miaka 27 na kuliunganisha taifa lake kwa kuvunjilia mbali ubaguzi wa rangi nchini humo. Mapafu ya Mandela yaliharibika akiwa mfungwa alikopata maradhi ya kifua kikuu mwaka 1988.Pia ametibiwa kutokana na saratani ya kibofu cha mkojo na maradhi ya tumbo.Alikuwa akipokea matibabu nyumbani kwake mjini Johannesburg wakati hali yake ilipodhoofika na kupelekwa hospitalini Jumamosi. Daktari bingwa wa mapafu wa Afrika kusini Guy Richards amesema kujirejea kwa homa ya mapafu ni nadra sana hadi pengine kulikuwa na uharibu wa mapafu hapo mbeleni kwa mfano kama mgonjwa alikumbwa na kifua kikuu basi maeneo yaliyoharibiwa huwa yanashambuliwa na bakteria mara kwa mara. Mandela na mkewe Graca Machel Mandela na mkewe Graca Machel Homa ya mapafu yamkuba tena Mwezi desemba alilazwa hospitalini kwa siku 18.Baadaye mwezi Machi mwaka huu alilazwa tena na mwishoni mwa mwezi huo huo alilazwa kwa siku 10 akiugua homa ya mapafu. Mkewe Bi Graca Machel amekuwa kando ya kitanda chake hospitalini baada ya kukatisha ziara mjini London Uingereza.Bintiye Zindzi hapo jana alimtembelea babake hospitalini na kusema ni shujaa. Viongozi kutoka kwingine duniani akiwemo waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na afisi ya Rais wa Marekani Barrack Obama wametuma risala za kumtakia afueni ya haraka huku wapenzi wake wakimiminia ujumbe wa heri katika mitandao ya kijamii kutoka kila pembe ya dunia. Mwandishi: Caro Robi/afp/dpa Mhariri: Josephat Charo. DW.DE Mandela alazwa tena hospitali Rais mstaafu wa Afrika Kuisini Nelson Mandela na shujaa wa mapambano dhidi ya utawala wa ubaguzi amelazwa tena hospitali Jumamosi(08.06.2013) baada ya hali yake kuwa mbaya kutokana na kupata tena maambukizi ya mapafu. (08.06.2013) Mandela aendelea vizuri na matibabu Madaktari wanasema rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kulazwa tena hospitalini mjini Pretoria akiwa na maradhi ya mapafu. (29.03.2013) Tarehe 10.06.2013 Mwandishi Caro Robi Mhariri Josephat Charo Gawa Tuma Facebook Twitter google+ Zaidi Mrejesho: Send us your opinion Chapisha Chapisha ukurasa huu Permalink dw.de/p/18mey Makala zaidi Maandamano hayajasita Uturuki 11.06.2013 Polisi wa Uturuki wamefyatua mabomu ya kutoa machozi na kuwarushia maji waandamanaji katika uwanja wa Taksim kwa mara ya kwanza tangu tarehe 1 mwezi huu wakati maandamano hayo yalipoghubikwa na ghasia wanajeshi wa kenya katika mji wa Burgabo,Kismayo Mji wa Bandari wa Kismayo mikononi mwa Madobe 10.06.2013 Wapiganaji wanaomtii mbabe wa kivita Ahmed Madobe nchini Somalia wameimarisha nguvu za kuidhibiti bandari ya kusini ya Kismayo baada ya siku kadhaa za mapigano na makundi pinzani . Hati za siri za Marekani zafichuliwa 10.06.2013 Visa vya kuchunguzwa mawasiliano ya simu ndani na nje ya Marekani vinaikumba nchi hiyo na idara zake za upelelezi.Wizara ya ulinzi imethibitisha uchunguzi wa kupatiwa vyombo vya habari mpango wa siri kunasa mawasiliano Tarehe 10.06.2013 Mwandishi Caro Robi Mhariri Josephat Charo Gawa Tuma Facebook Twitter google+ Zaidi Tutumie maoni yako Chapisha Chapisha ukurasa huu Permalink dw.de/p/18mey 02_2012 Themenbild für Facebook eingestellt im Mai 2012 Kuwa shabiki wetu kwenye Facebook tujadiliane. 02_2012 Themenbild für Twitter Tembelea DW katika Twitter Tembelea DW katika Twitter Handy groß Bildrechte: Die Deutsche Welle hat von Barbara Gruber die uneingeschränkten Nutzungsrechte für die Bilder zum Thema Per SMS zum Erntehelfer erhalten. Autorin: Barbara Gruber Eingestellt August 2009 Huduma zetu kwa njia mbalimbali Tuma SMS kwa DW Destination Europe Kijarida Kijarida cha Deutsche Welle IDHAA YA KISWAHILI Matukio Duniani Matukio ya Afrika Matukio ya Kisiasa Magazetini Michezo Masuala ya Jamii Noa Bongo Miaka 50 ya DW Kiswahili Uchaguzi Mkuu wa Kenya 2013 Miaka 60 ya DW Media Center Moja kwa moja Vidio Sauti Picha HAZINA YETU Sikiliza Matangazo Ujumbe wa SMS Washirika Anuani Wafanyakazi KUJIFUNZA KIJERUMANI Kozi ya Kijerumani Kijerumani XXL Community D Kufundisha Kijerumani IJUE DW Kijarida RSS
Posted on: Tue, 11 Jun 2013 08:48:35 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015