SHUKRANI Jana ilikuwa ni siku ya kutunukiwa shahada yangu ya - TopicsExpress



          

SHUKRANI Jana ilikuwa ni siku ya kutunukiwa shahada yangu ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Safari hii ya elimu ilianzia pale shule ya msingi ITETE(1997) iliyoko Halmashauri ya Busokelo jimboni kwa Prof MWANDOSYA .Mnamo mwaka 2004 nilijiunga na shule ya upili Lufilyo, ambayo ilijengwa na wazi kwa ushirikiano mkubwa na Mhe Mbunge, Prof Mark Mwandosya. Nikiwa Lufilyo , sehemu ya historia kuu katika maisha yangu ilianza kujengeka.Ni kweli kwamba shari ni sehemu ya maisha, pia heri ni sehemu ya maisha , na hivi ndivyo ilivyo kuwa kwangu nikiwa Lufilyo sekondari. Naamini kuwa elimu ina maana pana sana lakini mpaka kufikia hatua ya Chuo maana ya elimu huendana na mtazamo wa mtu ama jamii. Mwaka 2008 nilijiunga na masomo ya kidato cha tano na sita , katika mkoa wa Mwanza wilaya ya Geita, sasa Mkoa wa Geita.Huko nilisoma Historia, Geografia ,Kiingereza na Uraia(GS).Nikiwa Geita sekondari nilibahatika kuwa kiongozi mkuu wa serikali ya wanafunzi zaidi ya wanafunzi 1000(kidato cha 1 hadi cha 6). Katika kutimiza imani yangu kuwa, mabadiliko niyapendayo , lazima yatakuja endapo nitakuwa sehemu ya maamuzi. Niliona kuwa, uongozi ungenipa fursa ya kiushiriki katika kutafuta suluhu juiu ya matatizo ya wanafunzi wenzangu. Kama mwanadamu, kuna muda uongozi wangu ulikuwa si wa kusifiwa na kila mtu, ni dhahiri kuwa, hakuna kazi kubwa , kama kuwa daraja. Kiongozi ni mfano wa kuigwa, ukiwa kiongozi katika taasisi kama SHULE , sifa nzuri ni kuwafurahisha walimu na wanafunzi. Lakini hakuna kazi ngumu kama kuwafurahisha wanafunzi na walimu wakafurahi, kuwafurahisha walimu na wanafunzi wakafurahi, kusimamia sheria na wanafunzi wakafurahi, kuvunja sheria na walimu wakafurahi. NIKIWA Kiongozi wa serikali ya wanafunzi makosa yangu yalinifundisha kuwa; Uongozi ni zaidi ya kufurahisha watu, uongozi ni kujenga mahusiano mema na watu kisha kufungua mianya ya kujadili namna ya utatuzi wa matatizo , wala si kujijengea tabaka la juu. Japo nilitunukiwa cheti cha uongozi bora na zawadi lukuki, lakini imani yangu inasema si muda wote nilitimiza mahitaji ya wanafunzi wenzangu, si muda wote nilitatua matatizo ya wanafunzi wenzangu kwa utashi. Hakika kama mwanadamu kuna siku na muda niliteleza.NAOMABA RADHI KWA WALE WOTE WALIOKWAZIKA KWA MAAMUZI YA KIUONGOZI CHINI YA UTAWALA WANGU GEITA SEKONDARI 2008-2010) Nilipofika Chuo kikuu cha Dar es salaam, sikuamua kwa dhati kuwa kiongozi, lengo lilikuwa ni kufananisha dhana mbili 1. Ili maamuzi chanya yatokee ni vema ukawa nje ya uongozi 2.Ili maamuzi chanya yatokee ni vema ukawa sehemu ya uongozi Mpaka sasa majibu ninayo. Jana nimetunukiwa shahada ya kwanza katika fani ya sayansi ya mambo ya kale, bado ninahoji sababu yangu kufurahia shahada hii? Elimu , ni nyenzo muhimu sana katika kupambanua changamoto katika maisha ya mwanadamu, nikiwa nasoma masomo juu ya jamii za kale, hakika watu wa kale waliweza kupembua mambo kwa kiwango cha hali ya juu kuliko sasa. Kabla ya ukoloni, viashiria vya ukoloni vilipingwa vikali na wazawa wa kiafrika, ukoloni ulipingwa na wazawa wa Afrika, jamii za kale zilitengeneza moto kwa kubuni, jamii za kale zilitengeneza silaha kwa mawe, tamaduni za kale zilitunza staha ya mwaafrika. Leo ni wangapi wakiishi kama wazungu huonekana wakisasa? Leo wanaopuuza tamaduni za kiafrika wanachukuliwaje kama siyo kusemwa washamba nini? Leo bidhaa ngapi ambazo tunatoa nje ya nchi bila kuthubutu kutengeneza? Leo elimu ya chuo ni chanzo cha vijana kuwa wanaharakati wali si chanzo cha kuwa sehemu ya watatuzi wa matatizo ya jamii. Mwl Nyerere aliposema, mtu anapoenda shule, ni sawa na mtu anayetumwa na kijiji kutafuta riziki ya kijiji kisha akirudi, atumie alichopata kwa manufaa ya wanakijiji.Leo hii elimu ya chuo hata mtu mwenyewe aliyeipata asipokuwa makini haimsadi vipi jamii itegemee nini kutoka kwa wasomi wa kileo????????????????????? Elimu yetu imekuwa ya kinadharia sana, mara nyingi nimekuwa nikisema, mtu anayeishia darasa la saba au kidato cha nne, kisha akienda VETA, baada ya miaka mitano wakikutana na aliyeenda kidato cha tano mpaka chuo kikuu, hakika aliyeenda VETA ataweza kuwa si mtumwa wa ajira ukimfananisha NA MSOMI wa CHUO KIKUU Napenda kutoa RAI kwa wahitimu wenzangu, elimu hii ni kitu muhimu , kwetu, kwa familia zetu na jamii kwa ujumla. Endapo hatutakuwa makini, elimu hii itakuwa ni chanzo cha umasikini hadi tunazeeka. Serikali ina nafasi yake katika kujenga mazingira ya ajira, lakini vijana tukubali kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii Elimu ni rasilimali ya pekee sana, wakati mali zingine zote hupungua kadri zitumikavyo, lakini , elimu huongezeka kadri itumikavyo, Mwenyezi Mungu akiamua kumwadhibu mwanadamu, basi atamnyima uelewa. NAJIULIZA MASWALI MENGI JUU YA NAMNA JAMII YANGU ITANUFAIKA NA ELIMU HII. HAKIKA NIMETUNUKIWA SHAHADA, LAKINI SIKUSHEREHEkEA maana NAJUA HUKO NIENDAKO NI KULE ELIMU INAKOTUMIKA, NITASHEREHEKEA MIAKA KADHAA BAADA YA KUTATHIMINI NAMNA NITAKAVYO INUFAISHA JAMII KUTOKANA NA ELIMU HII. HAKIKA ELIMU HII NI MUHIMU, IKITOLEWA KWA UFASAHA NA IKIPOKELEWA KWA UFASAHA NAWATAKIA MASOMO MEMA WANAOENDELEA NA MASOMO YA SHAHADA YA KWANZA. MUNGU IBARIKI UDSM, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Posted on: Sun, 17 Nov 2013 10:59:26 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015