SIMULIZI: CHURA NAMBA 20 MTUNZI: Ibrahim Gama SEHEMU YA KUMI NA - TopicsExpress



          

SIMULIZI: CHURA NAMBA 20 MTUNZI: Ibrahim Gama SEHEMU YA KUMI NA NANE 339. Swali hili bila shaka, Lataka kuthibitika, Mie nimekamilika, Au mwehu miamia! 340. Gari yapinda pembeni, Ni Kibaha Mkoani, Tunakanyaga mizani, Kupima twasubiria. 341. Kupima tunamaliza, Safari twaendeleza, Naamua kumjuza, Asije kuniambaa! 342, “Hakika mimi mgeni, Sijafika abadani, Mwenyeji yukituoni, Anakuja nipokea.” 343. “Sijuwi aishi wapi, Au ni mtaa upi, Ndiyo nikawa sikupi, Jina lake la mtaa!” 344. “Kwangu ni msamalia, Kapanga nisaidia, Mwisho tutapofikia, Mengine utayajuwa!” 346. “Sasa nimekuelewa, Mwanzo sikukutambuwa, Naiwe itavyokuwa, Mwisho utaniambia!” 347. Mjadala tukafunga, Mawazo tukayalenga, Mbele katika Luninga, Macho tukatumbulia. 348. Saa nane ya Mchana, Mombo ndiyo twaiona, Hapa hatukai sana, Kula na kuchimba dawa! 349. Ni dakika ishirini, Wote twarudi garini, Tuna shibe matumboni, Safari yaendelea. 350. Kumi ya alaasiri, Twahitimisha safari, Ninashuka kwenye gari, Mwenyeji namngojea! 351. Simu yangu inaita, Mfukoni naifata, Mwenyeji anitafuta, “Nishashuka” namwambia. 352. “Hebu geuka kulia, Nipo nakusubiria” Na mie naangalia, “Ohoo?!” Twashangilia. 353. Bwana anikimbilia, Nami namkumbatia, Tukawa tumetulia, Hivi kwa muda kadhaa! 354. “Poleni ndugu poleni, Mmefika karibuni, Hii ndo A ‘Towni’ Jiji lililotimia.” 355. “Kaka yangu samahani, Hawa ni wako wageni, Ila mie nina deni, Huyu bwana anajuwa!” 356. Yule dada atamka, Na sie tunageuka, Eti yeye anacheka, Huku atusogelea! 357. “Huyu akudai nini, Au nikiasi gani, Niambie Marijani, Hima nitampatia!” 358. Mwenyeji ninamwambia, “Si deni unodhania, Ni maneno kusikia, Ya kwangu na familia!” 359. “Tuingieni garini, Tukaongee nyumbani, Mmechoka safarini, Mtoto ataumia.” 360. “Naomba nipelekeni, Kwangu mie Kaloleni, Mpajuwe na nyumbani, Mnywe ijapo kahawa!” ITAENDELEA
Posted on: Sun, 18 Aug 2013 04:43:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015