SIMULIZI : MSAKO MTUNZI : CHARLES J LIGONJA SEHEMU YA SITA O714 - TopicsExpress



          

SIMULIZI : MSAKO MTUNZI : CHARLES J LIGONJA SEHEMU YA SITA O714 79 77 78 “Usijali, kuna mtu utakuwa nae na yeye ndiye atakae endesha, Gloria kamuoneshe atakachotakiwa kufanya kwa huyo jamaa”Niliinuka na kuingia chumba cha kushoto na baada ya muda niliulizwa kama nilifanyiwa unyago kipindi nimevunja ungo. “Kwanini unaniuliza hivi dada?” “Unatakiwa kutoa jibu hakuna jingine,kama ulivyokuwa ukimjibu bosi na ndivyo unavyotakiwa kujibu maswali yangu” “Ndio nilifanyiwa” “Basi ni hivi..”huyo dada niliyekuja kumfahamu kwa jina la Jamila alikuwa mtundu hasa,aliniambia kuna baadhi ya maeneo kuingia lazima kutumia miili yetu kutokana na ugumu wa hao wahusika kwenye masuala ya pesa na mimi unavyoniaona Arusha wanaume wengi ambao tunafanya nao biashara wamenichoka hivyo basi nafasi yangu unaichukua wewe nikiwa na maana ukiona mtu anakusumbua basi mpe penzi tena zito mpaka mwenyewe alegee na ndio mafanikio yako bila kufanya hivyo inakuwa ngumu kufanikiwa. “Niweke wazi kwani biashara gani tunaenda kuifanya?” “Bosi atakueleza badae ukiwa tayari kuelezwa lakini pia mpaka akuone kama uko makini na kazi ama la!”Niliendelee kubaki gizani. Mazungumzo yalimalizika na badae tukatoka mpaka alipokuwa bosi na baada ya kupewa taarifa kuhusu mimi wote tuliinuka na kuondoka,tuliingie eneo ambalo sijawahi kuwaza hata siku moja kama naweza kuingia hotel 9Serena hotel) nzuri kama ile katika maisha yangu,tulikula na kunywa kadri ya uwezo wetu na ilipofika saa kumi na mbili tuliondoka na kwenda moja kwa moja mpaka mbezi ya kimara ambako saa mbili usiku safari ya kwenda Arusha ilianza,nilikabidhiwa begi jeusi lenye maneno na herufi zile zile (UK na NUGA) nakuambiwa hiyo ni mali yangu lazima niitunze mpaka tunafika Arusha ambapo baada ya muda mfupi tutakuwa kule kutokana na aina ya gari ambalo tulikuwa tukilitumia,mwendo kasi unaua ndio vibao ambavyo vilikuwa vikisomeka njiani lakini hilo halikumzuia Karim kuendesha kwa kasi ya ajabu,madirisha yalikuwa yamefungwa kiyoyozi kikachukua nafasi yake kwani hapo mwanzo nilipoona ubaridi mzuri sikuwa na jibu la wapi huo upepo unatoka wakati vioo vimepandishwa mpaka juu,mwendo ulitisha sana. Saa sita usiku tuliingia mjini Arusha,mawazo yangu yalienda moja kwa moja kwa Maganga lakini sina uhakika kama nitapata hata muda wa kwenda kumtafuta na kweli ilikuwa hivyo kwani usiku huo tuliingia kwenye jumba kubwa na nilipoingia kwenye hilo jumba mawazo yalirudi nyuma haraka sana na kukumbuka tuliyoongea jana yake,kama nilifundwa nami kushangaa kwa swali hilo na nilipoingia kwenye hilo jumba nikajua labda nitakutana na jaribio hilo na kama nitashindwa kutatokea nini lakini tofauti na nilivyowaza mambo yalikuwa sawa na baada ya kukabidhi mzigo tulipumzika kidogo na ilipofika saa kumi alfajiri safari ya kurudi Dar es salaam ikaanza. Nora haya sina uzoefu nayo,kusafiri usiku kucha,umbali mrefu tena mwendo wenyewe ikitokea ajali hakuna wa kupona jamani maisha haya,nilikuwa na usingizi na kuamua kulala ili angalau niwe na hali nzuri kwani sijui nitakutana na nini nikifika Dar es salaam. Saa tatu asubuhi tulikuwa Sinza,bosi alikuwepo ofisini na kweli baada ya muda mfupi badae alituita na kutupatia pesa kwa ajili ya kazi tuliyoifanya,kila mmoja alipewa laki tano na kutuacha tukapumzike. Nora mikononi mwa Charles,maisha yamebadilika anaweza kushika million mfukoni mwake,alikuwa na uwezo wa kupanga chumba na kununua vitu vya muhimu kwa mwanamke wa kisasa,Nora alikuwa tofauti kwani aliweza kuanza kujitengenezea maisha.Siku nazo zilizidi kusonga mbele na mwisho wa siku Nora alipelekwa shule kwa ajili ya kujifunza kiingereza na kweli alipikwa akapikika,Nora akawa tayari kwenda hata nje ya nchi kwani lugha haikuwa tatizo kubwa ingawa hakuwa anajua kuongea kwa kiwango cha juu lakini ulikuwa huwezi kuteta jambo asikusikie,Nora ameingia kwenye mtandao wa kuuza dawa za kulevya. Haikuwa rahisi siku ya kwanza anaingia kwenye ndege kwa ajili ya kwenda nchini Pakistan kwa ajili ya kwenda kubeba mzigo na kweli baada ya siku mbili anafika kwenye kijiji ambapo anapokelewa na bibi kizee ambae anampeleka shimoni na alipofika huko alipewa mzigo,hakukuwa na maswali mengi kila kitu kilishafanywa na Charles ambae alikuwa nchini Tanzania,nazibebaje swali gumu hana wa kumpa jibu zaidi ya karatasi aliyopewa ikimuonesha wapi anatakiwa aende akameze mzigo,kazi imeanza !? Alirudi mpaka alipoelekezwa na kukutana na vijana wengine toka Afrika ya Mashariki, wengi wakiongea Kiswahili lakini wasichana walikuwa wachache sana na hapo ndipo nilipokutana na Deo ambae kwa muda mrefu nilikuwa sijaonana nae pale ofisini. “Nambie Deo?” “Poa, karibu sana” “Umekuja lini huku?” Kabla sijajibiwa alinionesha ishara nimfuate na kweli niliinuka na kwenda alikotaka twende,tulipanda teksi na kutupeleka mpaka kwenye nyumba ya kulala wageni na tulipofika pale kazi ilikuwa moja tu kuandaa ule unga na kuufunga katika vifungashio maalum na badae kuanza kumeza ili safari ianze siku ya pili,ilikuwa kazi ngumu sana kwangu lakini kutokana na shida ambazo nimezipitia niliamua tu kujilipua liwalo na liwe,mdomo wote ulikuwa mwekundu kutokana na damu nyingi iliyokuwa ikinitoka kutokana na kumeza zile kete. “Ndio kazi unayoifanya?” “ Sio swali,hapo piga mstari kwani bila hivyo mambo hayaendi dada yangu” “Mh! Ila jera mkononi kwani hii biashara inapigwa vita sana na serikali yetu” “Kama umeamua kujilipua, mambo ya jera yapo ingawa bosi yuko makini sana na kuna watu wengi wenye nafasi za juu serikalini kisha washika ndio maana hatuna wasiwasi sana lakini umakini lazima” Deo aliongea kwa kujiamini. Nora mwenye maswali mengi,huo umakini unaosisitizwa ni wa aina gani,mbona ananichanganya namna hii na kibaya zaidi ananiambia mimi nae nimeaminiwa sana na bosi kwani kuna wengine wanafanya kazi za bosi lakini hawajawahi kuonana na bosi,wao huiishia kutumwa,wanabeba mzigo na kuufikisha sehemu fulani na hapo wanaambiwa wauache kuna mtu atauchukua na kweli wakiingia hasa hotel kubwa kubwa jijini Dar es salaam hukutana na pesa zao ziko pale,kuchukua anakuja kuchukua nani hilo sio lao tena na anaekuja kuchukua hamjui bosi anaambiwa aende sehemu fulani atakutana na gari nyeusi imepaki atupie mzigo kwenye buti ambalo akifika hilo eneo atalikuta hilo gari na buti litakuwa wazi yani kwa kifupi ni kazi ya kimafia sana na hao ambao hawamjui bosi wengi wao wamekamatwa na kufungwa kwani wanashindwa kueleza hasa aliyewatuma lakini pia kuna waliokuwa wakijaribu kukimbia na mzigo nao hawakufika mbali waliweza kunasa kwenye mkono mrefu wa Charles na kupigwa risasi,ilitisha sana! Majuto mjukuu tayari Nora ameingia kwenye mkono hatari, mkono wa kifo, kaweka maisha yake rehani,hana pa kutokea na hana wa kumuomba ushauri kwani hata kuwa na Deo katika nchi za watu ni kutokana na ugeni wake lakini mara zijazo itabidi awe peke yake kwani haitakuwa vyema kupoteza huku na huku,hilo kwa Charles hakutaka litokee hata siku moja ingawa hasara alishaingia mara nyingi lakini anachojali kwa sasa ni faida. “Twende kumekucha” Ilikuwa sauti ya Deo ambae muda wote nikiwa kwenye lindi la mawazo mwenzangu alikuwa amelala, nilijifuta uso na safari ikaanza, zilikuwa njia za polini saa kumi usiku na baada ya muda mfupi badae tulikutana na vijana wengi kwenye hiyo njia wote tukiwa njiani kuelekea kunako njia za panya ili tupate usafiri ambao utatufikisha uwanja wa ndege na kupanda ndege ambayo itatufikisha nchini Afrika kusini baada ya hapo kupanda ndege nyingine mpaka Tanzania ni safari ya siku mbili,tulipofika Afrika kusini kazi ilishafanyika,njia ilikuwa nyeupe tukaingia kwenye ndege tayari kwa safari ya kurudi Tanzania,koo likiwa na hali mbaya sana baada ya kutoa kete kwa haja kubwa na kusafisha na badae kuvimeza tena,kazi ngumu sana na inahitaji moyo wa ujasiri,inahitaji mtu aliyejikataa kufanya kazi kama hii,Nora hakujua kama nae amejikataa ama vipi lakini yote aliyakabidhi mikononi mwa Mungu,ama kweli hata wahalifu wanamkumbuka Mungu,kumbe Mungu ni wa wote,kazi kweli kweli. Baada ya saa kadhaa angani tulisikia kipaza sauti kikitutaka tufungue mikanda kwani tayari tulikuwa kwenye ardhi tulivu ya Tanzania lakini yanayofanyika kwenye hiyo nchi makubwa sana, vijana wanatumiwa kama punda kuingiza madawa ya kulevya na hata kuyatumia na kuneemesha wenye nazo ambao nguvu zao hazishikiki, vijana wadogo wanapoteza maisha kutokana biashara hiyo,inauma lakini!Wakiwa kwenye ndege ndio wakati ambao Deo aliweza kumsimulia namna gani Charles alipata utajiri. “Jamaa alipambana sana kuhakikisha anapata pesa,baada ya kumaliza kidato cha nne shule ya sekondari Kwiro Charles alianza biashara ya kununua mazao toka kwa wakulima na badae kuyauza,alifanya hivyo kwa muda wa miezi mitano na badae alijiunga na shule ya sekondari Meta iliyoko jijini Mbeya ambapo alipofika huko alianza kuuza bangi,alikuwa akienda Arusha na kununua bangi na kuileta Mbeya na nyingine kupeleka Dar es salaam,hakuacha shule ingawa alikuwa mtegaji mkubwa na kuanzia kipindi hicho tayari alishaanza kula na walimu hasa mwalimu wake wa darasa,alikuwa akiondoka mpaka mwezi mzima na akirudi humpatia mwalimu laki moja au mbili ili amlinde na hayo ndiyo yalikuwa maisha yake. Miaka miwili haikuwa mingi,Charles alimaliza shule na kuingia jijini Dar es salaam ambako alishakuwa na chumba chake maeneo ya Sinza,aliendelea na biashara yake,matokeo yalipotoka alipata daraja la pili na kuomba kujiunga chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) hapo sasa ndipo alipoweza kujipanua katika kazi zake. Baada ya miezi miwili alianza safari za kwenda Kagera hasa wilaya ya Ngara,hakuna aliyejua kilichokuwa kikimpeleka lakini kikubwa alikwenda kuona namna gani anaweza kuingia kwenye biashara ya kuuza siraha akiamini itamtoa haraka. “Siraha!” “Muone vile vile,jamaa mafia!” Biashara ya siraha haikuwa rahisi kama alivyotaka,alikuwa akinunua siraha kutoka kwa Wanyarwanda na kusafiri nazo mpaka Dar es salaam kuja kuuza kwa majambazi,angalia kwenye benki nyingi matukio yalikuwa yakifanyika na majambazi wakiwa na siraha kubwa kubwa basi hiyo kazi ya Charles,alikuwa akiingiza siraha kali za kivita ikiwemo short machine gun (SMG),bastola na nyinginezo nyingi,hakukomea hapo kwani nae alitengeneza kundi lake na kuanza kufanya matendo ya kijambazi ikiwemo kuteka magari,alianza na kuteka mabasi ya mikoani. YALIYOJIFICHA YANAANZA KUTOKA NJE,KAA MKAO MWINGINE UONE KESHO MAMBO YATAKUAJE. HESHIMA KWA WOTE MNAENDELEA KUSOMA KAZI ZANGU,LIKES NA COMMENTS ZINANIPA NGUVUYA KUANDIKA ZAIDI NA ZAIDI.
Posted on: Sat, 14 Sep 2013 07:11:56 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015