SOMO: Sifa Za Nabii Mtumishi mwenye Huduma Ya Unabii ndani yake - TopicsExpress



          

SOMO: Sifa Za Nabii Mtumishi mwenye Huduma Ya Unabii ndani yake , ni lazima awe na maneno yafuatayo ndani yake ambayo yanampa sifa za yeye kuwa Nabii. i. Ni lazima awe na karama za mafunuo ndani yake, ambazo ni; karama ya neno la maarifa, karama ya neno la hekima, karama ya kupambanua roho. ii. Ni lazima ndani yake awe na karama za kunena, ambazo ni; karama ya Unabii, karama ya aina za lugha, na karama ya tafsiri za lugha…. 1Korintho 12:8,10…” Maana mtu mmoja Kwa Roho apewa neno la hekima; Na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye Yule……. Na mwingine matendo ya miujiza, na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; na mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha”. iii. Nabii ni lazima awe na uwezo katika Mungu kufunua maneno ya fumbo, kutafsiri ndoto, na kufunua mafundo yatakapotukia. Danieli 5:12…”kwa kuwa roho njema kupita kiasi na maarifa,na ufahamu,na uwezo wa kutafsiri ndoto,na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo zilionekana katika Danieli…………”. iv. Ni lazima awe na nuru ya ufahamu katika macho yake ya rohoni, ili kumsaidia asidanganyike, na aweze kuchanganua, kuchambua kwa ufasaha kile anacho kiona na kukisikia ili kupata ufafanuzi na majawabu sahihi. Efeso 1:18 “Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru,mjue tumaini na mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wake katika watakatifu jinsi ulivyo”. v. Awe na uzoefu katika kuongozwa na Roho mtakatifu, hasa katika yale anayofunuliwa kila wakati, aweze kuelekea kwa kila maelekezo anayoelekezwa, anayoonyeshwa na kufundishwa. Warumi 8:14…” Kwa kuwa wote wanao ongozwa Na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu”. vi. Nabii ni lazima awe na uzoefu katika kutokewa na Mungu,Yesu, Roho Mtakatifu au malaika, na jinsi ya kuhojiana naye, bila kubabaika au kudanganyika. vii. Ukiwa na kipawa cha unabii ni lazima uwe na uzoefu wa kuhojiana naye,(Mungu Aliye Hai) ili unapotoka katika mafunuo uwe na maelezo thabiti, na majibu ya uhakika. Kutoka 3:1-4 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro kwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu,hata horebu. Malaika wa BWANA akamtokea,katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto,nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema nitageuka sasa niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei. BWANA alipoona ya kuwa amegeuka,ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema ;Musa!, Musa! Akasema mimi hapa”. Kama Kanisa Unalosali Huduma Ya Unabii Haipo: Neema hii ya Huduma ya Unabii, ni huduma ya muhimu sana Kanisani, na kwa mwili wote wa Yesu Kristo. Na siyo salama kukaa kanisani bila huduma hii. Na kama nilivyotangulia kusema hapo awali,… ikiwa hauioni huduma hii kanisani, muulize mchungaji wako au Askofu wako, akueleze kwa ukanuni. Maana ni neno la hatari kuliko unavyofikiri. Na usalama wa kanisa hilo ni mdogo sana. Kwa kuwa shetani atapanga lolote baya dhidi ya kanisa na kuwaweza kama atakavyo, maana macho ya rohoni (Huduma ya Unabii) haipo. Jaribu kufikiri hivi; nchi yoyote ikikaa bila rada (chombo kinacho kagua na kulinda anga), unadhani nchi hiyo iko salama kweli? Hata ujifariji kiasi gani, na ukatumia maandiko yanayokufurahisha wewe, ni neno la hatari sana. Kipawa cha Unabii ni kama kifaa cha rada kinachoangalia usalama wa Kanisa la Yesu Hapa duniani. Kwa ajili hii muulize kiongozi wako wa Kanisa Kama anaweza kukufundisha. Kama anaweza kufundisha, mwombe akusaidie wewe binafsi pamoja na kulifundisha Kanisa lote. Kama hawezi basi mwombe atafute mwalimu anayeweza kufundisha maneno haya ya Unabii, ili aje hapo kanisani kufundisha. Kama huduma hii imeanza kuchipua ndani yako, tafuta waalimu wenye neema ya kufundisha maneno haya ili usaidike kwa usalama wa huduma hii, ya unabii uliyo ndani yako, ili ukue na upige hatua kiroho,kiutumishi na wito uliyo ndani yako. Faida Za Huduma Ya Unabii Huduma ya Unabii katika mwili wa Yesu Kristo hapa Duniani, inafaida zifuatazo: 1. Huduma ya unabii inasaidia kugundua hatari au tatizo litakalompata mwanadamu, Kanisa, au Huduma Fulani inayomwamini Yesu ili kuwasaidia waweze kuepuka au kupona na kuwa salama, dhidi ya mashambulizi ya shetani. 2Falme 20:1-5 “Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya nabii, mwana wa Aamozi,akamjia akmwambia, BWANA asema hivi, tengeneza mambo ya nyumbani kwako maana utakufa, wala hautapona.Baasi Hezekia akajigeuza, akelekeza uso wake ukutani, akamwaomba Bwana akasema. Nakusihi . BWANA ukumbuke sasa jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli, na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia aklia sana sana. Ikawa kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati,neno la BWANA likamjia na kusema,Rudi ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako, asema hivi, nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi, yako;tazama nitakuponya, siku ya tatu utapanda nymbani kwa BWANA” 2. Faida ya pili ni hii; Tunapata kibali cha kuyajua mafumbo na siri za Ufalme wa Mbinguni. 1Korintho 2:10. “ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu”. 3. Kupitia huduma hii ya Unabii,inatusaidia kuwa watu wa rohoni,na kupata ufahamu wa kujua na kufahamu mambo yote katika hekima ya hali ya juu sana. 1Koritho2:15…” Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. 4. Huduma ya unabii inatusaudia kujua siri za ufalme wa mbinguni, ili tukue kiroho. Mathayo 13:11. “Akajibu akawaambia, ninyi m’mejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mbinguni, bali wao hawakujaliwa” 5. Unabii ni jicho la kiroho linalomwezesha mwanadamu,kuona siri za ulimwengu wa roho. Ufunuo 1:10,11.” Nalikuwa katika Roho siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu,kama sauti ya baragumu ikisema,haya uyaonayo uyaandike katika chuo,uyapeleke kwa makanisa saba………. 6. Unabii unatusaidia kujua siri za shetani, ili tujue namna ya kujipanga, na kujiandaa ili tuweze kuzidhibiti hila zake, silaha zake na mitego yake, kwa jina la Yesu. Ayubu 33:22-24… “Naam nafsi yake inakaribia shimoni, Na uhai wake unakaribia waangamizi. Kwamba akiwapo malaika pamoja naye, mkalimani, mmoja katika elfu, Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo; Ndipo amwoneapo rehema na kusema, mwokoe asishuke shimoni, mimi nimeuona ukombozi”. 7. Unabii unatusaidia kuzijua siri za wanadamu, mawazo yao, jinsi wanavyotuwazia, namna wanavyotusengenya, na kila jambo lolote ambalo wanadamu wenzetu wamelipanga dhidi watumishi au kanisa. 1Korintho 2:11… “Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake?Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayajuaye ila Roho wa Mungu” 8. Huduma ya unabii inatusaidia kuzijua siri za Roho Mtakatifu, na yale tuliyokirimiwa na Mungu aliye hai, ambayo yako ya AHADI ZA MUNGU, na yale yaliyo katika haki zetu, ambyo tuliyapewa tangu tumboni. 1Korintho 2:12…” Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia , bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliokirimiwa na Mungu. 9. Huduma ya Unabii inatusaidia kuwa wakamilifu au waliokomaa kiroho katika wokovu na utumishi, Efeso 4:10-13 “ Naye aliyeshuka, ndiye aliyepaa, juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote, naye alitoa wengine kuwa Mitume,na wengine kuwa manabii,Na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na Waalimu, kwakusudi la kuwakamilisha wata katifu, hata mwili wa Kristo ujengwe,” 10. Aidha Huduma ya unabii hulisaidia Kanisa kufikia katika cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. Na kulifanya Kanisa kuwa katika kiwango cha juu sana kiroho na kihuduma. 11. Aidha malaika mkalimani kutoka mbinguni, anawasaidia sana Manabii kuweza kuchambua na kupambanua, yale yanayoonekana katika ulimwengu wa roho au wa mwili. Ayubu33:23 “Kwamba akiwapo malaika pamoja naye Mkalimani, m’moja katika elfu,ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo” 12. Unabii unafanya kazi ya kuleta taarifa kuhusu maisha ya mwanadamu, na yale yatakayompata hapo baadaye katika maisha yake ya kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho. Mwanzo37:9…
Posted on: Thu, 15 Aug 2013 16:40:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015