SURA YA NANE URATIBU WA MAHUSIANO YA WASHIRIKA WA - TopicsExpress



          

SURA YA NANE URATIBU WA MAHUSIANO YA WASHIRIKA WA MUUNGANO 102.(1)Kutakuwa na Tume ya kusimamia na kuratibu mahusiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano na kusimamia na kuratibu mahusiano baina ya Serikali za Washirika wa Muungano, ambayo itajulikana kwa kifupi kama “Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali”.(2) Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali itaundwa na wajumbe wafuatao: (a) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Rais wa Tanzania Bara; (c) Rais wa Zanzibar; (d) Mawaziri Wakaazi; (e) Waziri mwenye dhamana ya mambo ya nje wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 103. Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali itakuwa na malengo yafuatayo: (a) kuweka utaratibu borana endelevu wa mashauriano na mashirikiano baina ya Serikali ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano; (b) kukuza na kuwezesha uratibu na mashirikiano miongoni mwa Washirika wa Muungano kuhusu masuala yasiyo ya Muungano kwa lengo la kuwezesha kufanana kwa kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote; (c) kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya Serikali ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano kujadili juu ya utekelezaji wa mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano kwa manufaa na ustawi wa wananchi wote; na (d) kuweka mazingira mazuri ya utatuzi wa migogoro baina ya Serikali ya Muungano na Washirika wa Muungano. 104.-(1) Tume ya Mahusiano na Uratibu ya Serikali itakuwa na jukumu maalumu la kuwezesha uratibu na ushirikiano katika kutekeleza masharti ya Katiba hii, sera, sheria, mipango na mikakati baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano na baina ya Serikali za Washirika na pia itakuwa chombo maalumu kwa ajili ya: (a) mashauriano na mashirikiano baina ya: (i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano; na (ii) Serikali za Washirika wa Muungano zenyewe katikamasuala yasiyo ya Muungano; (b) kusimamia, kuratibu na kuhakikisha kwamba kuna kuwiana kwa sera na sheria za Washirika wa Muungano katika masuala yasiyo ya Muungano; (c) mashauriano na ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano na taasisi za kimataifa kwa niaba ya nchi; (d) usimamizi na ukuzaji wa masuala yenye maslahi kwa Taifa; (e) usuluhishi na utatuzi wa migogoro baina ya: (i) Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano; na (ii)Serikali za Washirika wa Muungano katika masuala yasiyo ya Muungano; (2) Kwa madhumuni ya Ibara ndogo ya (1)(e), endapo upandewowote katika mgogoro hautaridhika na uamuzi wa Tume ya Mahusiano na Uratibu wa Serikali, unaweza kukata rufani katika Mahakama ya Juu na uamuzi wa Mahakama hio utakuwa ni wa mwisho. (3) Bunge linaweza kutunga sheria kwa ajili ya: (a) kusimamia mahusiano na uratibu baina ya Serikali za Washirika wa Muungano na kati yaSerikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali za Washirika wa Muungano; na (b) kuweka utaratibu wa utatuzi wa migogoro kwa mujibu wa Ibara hii.
Posted on: Fri, 30 Aug 2013 10:06:22 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015