Siku ya Jumanne ya tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2001, ndege ya - TopicsExpress



          

Siku ya Jumanne ya tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2001, ndege ya Marekani namba AA Flight 11 ilivamiwa na magaidi watano na kutekwa angani ikiwa na abiria 76 na wafanyakazi 11 na kisha magaidi hao kuiongoza ndege hiyo kugonga jengo la World Trade Center ambapo ililipuka na kuvunja jengo hilo pamoja na kuua abiria wote waliokuwa ndani yake wakiwemo walioiteka. Lakini kuna watu wawili ambao ilikuwa wawepo kwenye ndege hiyo ila hawakuwepo. Seth MacFarlane (Mtunzi wa show ya Family Guy) na Mark Wahlberg (Mwigizaji maarufu nchini Marekani). Wote walikuwa wameshakata tiketi kusafiri na ndege hiyo. Wahlberg alibadili safari dakika ya mwisho bila hata mwenyewe kujielewa na kuelekea jijini Toronto nchini Canada na MacFarlane alichelewa uwanja wa ndege kutokana na kunywa pombe nyingi jana yake usiku na kufika dakika 10 baada ya ndege kuondoka. Somo: Mungu ndiye mwenye mpango na maisha yako na atakuvusha na kila jambo kwa namna anayojua Yeye.
Posted on: Tue, 09 Jul 2013 03:12:27 +0000

Trending Topics




© 2015