TFF YAIPIGA STOPU TIMU ‘FEKI’ TOKA NIGERIA!! JANA ILIKUWA - TopicsExpress



          

TFF YAIPIGA STOPU TIMU ‘FEKI’ TOKA NIGERIA!! JANA ILIKUWA ICHEZE NA YANGA, KISHA COASTAL, MBEYA CITY!! KATIBU MKUU wa TFF, Angetilie Osiah, amesema wamefuta Mechi za Klabu kutoka Nigeria, FC 3 Pillars, walizokuwa wacheze Nchini baada ya Shirikisho la Soka la Nigeria, NFF, kusema haijui lolote kuhusu Timu hiyo na Ziara yake. Kwa mujibu wa Osiah, imebidi TFF waifute Ziara hiyo ya Klabu hiyo ya Nigeria kwa sababu Kanuni za FIFA haziruhusu Timu kucheza nje ya Nchi zao bila Kibali toka kwa Mamlaka ya Soka ya Nchini kwao. Vile vile TFF imesema FC 3 Pillars haijapandishwa Daraja kucheza Ligi Kuu ya Nigeria, NPL [Nigeria Premier League] kama vile tamko la Waandaaji wa Ziara yao Nchini, SportLink International, walivyodai kwenye Matangazo yao. Jana FC 3 Pillars ilikuwa icheze na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na pia Timu hiyo ilipangiwa kucheza na Coastal Union na Mbeya City, ambayo Msimu huu unaokuja itacheza Ligi Kuu Vodacom baada ya kupanda Daraja. Licha ya kuifuta Ziara ya FC 3 Pillars, pia Katibu Mkuu wa TFF, Angetiilie Osiah, alibainisha kuwa hata hao Waandaaji, SportLink International, hawajasaliwa na FIFA kwa ajili ya kuandaa Mechi za Kimataifa kama vile taratibu zinavyotaka. Aokiongeza, Osiah alivitaka Vyama vya Soka vya Mikoa viwe waangalifu wasidanganywe na Wajanja wanaoleta Timu toka nje bila ya kufuata taratibu zilizowekwa.
Posted on: Fri, 19 Jul 2013 06:41:00 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015