Tripoli Maelfu ya wananchi wa Libya wameandamana huko Tripoli mji - TopicsExpress



          

Tripoli Maelfu ya wananchi wa Libya wameandamana huko Tripoli mji mkuu wa nchi hiyo wakishinikiza kuitishwa uchaguzi wa bunge. Maandamano hayo yametokea Novemba 10 mwaka huu ambapo maelfu ya wakazi wa mji mkuu Tripoli wameshiriki kwenye maandamano wakitaka kufanyika uchaguzi mpya wa bunge nchini humo. Wafanya maandamano hao wamesisitiza kufanyika uchaguzi mpya wa bunge kwa mujibu wa mfumo wa wagombea binafsi bila ya kufungamana na chama au kundi lolote na kuundwa serikali ya kutatua migogoro hadi hapo itakapomalizika kazi ya kuandaa rasimu ya katiba mpya ya Libya. Wakazi hao wa mjini Tripoli wamefanya maandamano hayo katika kujibu wito uliotolewa na kundi la wanaharakati lijulikanalo kwa jina la harakati ya Novemba Tisa. mwakilishi wa harakati hiyo ya Novemba Tisa Abdallah al Muhammad Novemba 9 mwaka huu alisema kuwa harakati hiyo imeasisiwa ili kupinga kuendelea kufanya kazi baraza la Congress ya taifa ya Libya na kutaka kufanyika uchaguzi mpya wa bunge ambapo harakati hiyo iliasisiwa na vijana kadhaa wa Libya katikati ya mwezi uliopita wa Oktoba.
Posted on: Mon, 11 Nov 2013 05:58:19 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015