UCHAMBUZI WA KIUCHUMI; KAGAME Vs KIKWETE - TopicsExpress



          

UCHAMBUZI WA KIUCHUMI; KAGAME Vs KIKWETE ----------------------------- Nimekuwa nafuatilia huu mgogoro kati ya Rwanda-PK vs Tanzania-JK. Kuna issue haijaguswa bado na ninaona baadhi ya Jirani zetu wanaonesha nia ya kutaka kuudandia ktk mitandao ya kijamii 1. Watanzania wanaokosoa kwa nn JK aliongea sielewi wanatumia base ipi kusema hayo. Kwani RAIS wetu anapokwenda kwenye vikao vya kimataifa kama EAC, AU au UN, haruhusiwi kuchangia mada? Katiba au miongozo yetu inatakiwa awe bubu kwenye vikao? Tunapojadili suala la Rwanda inatakiwa tuweke pembeni mapungufu ya Ndani ya JK tumjadili on this particular issue. Tusiwe general kuchukua mapungufu yake ktk wizara au taasisi za ndani ndio iwe locus stand yetu ya kwa Kila suala atakalofanya. Ana mazur na mabaya yake Kila moja lizingatie muktadha husika. 2. Tatizo ni Uchumi. Naona wakenya nao wanajiingiza kwenye huu mgogoro ha ha ha. Issue ipo hv. Rwanda wamekuwa wanawasapoti waasi mashariki mwa Congo kwa mud mrefu Rwanda na PK wamekuwa wanaaiba maliasili kule Rwanda kwa muda mrefu. Sasa Tanzania kupeleka jeshi lake chini ya makubaliano ya. AU na UN imekuwa tishio la kiuchumi kwa jirani zetu kwa muktadha huu. Kama Congo patakuwa na Amani basi PK na jeshi lake hawataendelea kuiba mali Congo. Badala yake kijiografia na kisiasa Tanzania itanufaika kwa kufanya biashara na Congo kuliko nchi yoyote ile ktk maziwa makuu na Afrika mashriki. Ikumbukwe kama Congo kutakuwa na aman basi Congo kuna malighafi na maliasili nyingi na soko kubwa kuliko nchi yoyote sub Saharan Africa. Ili Tanzania kujinufaisha kiuchumi na kibiashara na Congo; yafuatayo yanafanywa amabayo ni tishio kwa wenzetu; A. Tanzania imekuwa kinara wa kupigania amani na kuisha kwa uhasama nchini Congo. B. Tanzania inajenga uwanja wa kimataifa mkoan kigoma ili ndege kubwa zinazotoka na kuingia Congo kwenda Dubai na kwingineko zitue pale kigoma kwa sababu za kibiashara C. Tanzania itafadhiliwa na china ili kujenga bandari kubwa kuliko zote ukanda huu wa pwani ya masharik ya Afrika. Hapa Kenya ndo wanaanza kuweweseka wanaona ni pigo kwa mradi wao wa Bandar ya Lamu D. Tanzania kupitia china wanaboresha reli ya Tazara na reli ya kati lengo ni kufanya Tanzania kuwa gateway ya central Africa landlocked countries. Ikumbukwe hata hao Rwanda na Uganda wana mradi wa reli isaka via Burundi to Rwanda. Pia Uganda wanataka bandari ya Tanga iboreshwe ili waitumie wao na reli ijengwe kutoka Tanga mpaka Mji mojawapo katika mwambao wa ziwa Victoria kule Uganda E. ikumbukwe Zambia wanafanya biashara zao kupitia bandari ya dar. Kwahiyo ktk miaka 10-20 ijayo kama miradi hii itafanikiwa na kutumiwa vizur na Tanzania, basi ni dhahiri shahiri uchumi wa Tanzania utakuwa tishio kwa Kenya amabao nao wanaanza kupagawa kumuunga mkono PK. Kwani Tanzania itanufaika kibiashara Zambia, Burundi, Uganda, Congo na hata huyo PK Tanzania ni viable entry/exit point yake kwa bandari kuliko Mombasa. F. Ukinzingatia mchanganuo huo na upatikanaji wa gesi, mafuta, makaa ya mawe, misitu, n.k Pamoja na Tanzania Geopolitical position Yake. China wanaona inalipa kuwa mshirika na Tanzania. America ameshituka nae anataka kuwa mshirika zaidi na Tanzania. Vile vile brazil na nchi zingine. Kwahiyo hata uhusiano wa kimataifa wa Tanzania utakuwa mzuri. Ikumbukwe hao marekani na western power ni wagomvi wakubwa wa Rwanda hv karibuni na tishio la uhuru wa Kenya ktk masula ya kupelekwa ICC, hali ikiwa hivyo ndo kwanza watu hao western power wanakula na kulala Tanzania. Kwahiyo hakuna option ni kwa Kenya na Rwanda kuaanza kutuchukia Tanzania. Ndio mwezi ulopita wakakutana pale uganda, museve, kageme na uhuru. Ni viajjenda vya kutushia kuhamisha baadhi ya miradi kutoka Tanzania kwenda Kenya na Uganda. Kwa ufupi niishie hapa Sintoshangaa ukisikia Kenya nao wanaopeleka jeshi Nchini Congo
Posted on: Sun, 04 Aug 2013 06:03:37 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015