ULIMWENGU WA KIISLAM Mawaziri wa fedha na viongozi wa benki kuu wa - TopicsExpress



          

ULIMWENGU WA KIISLAM Mawaziri wa fedha na viongozi wa benki kuu wa kundi la nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda na zinazoimarika kiuchumi duniani G20 wameazimia kuunda nafasi za ajira na kukuza uchumi zaidi ya kutoa nafasi katika hatua za kubana matumzi. Tangazo hilo linafuatia mkutano wao wa siku mbili, uliyofanyika mjini Moscow nchini Urusi. Lakini Waziri wa Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ameonya kwamba nidhamu katika bajeti za nchi ni jambo lisilopaswa kusahaulika. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moscow Schäuble amezungumzia mipango ya Ujerumani ya kukuza ajira na ukuaji wa uchumi lakini pia alisema hali hiyo haiwezekani bila ya uwezo wa kifedha kupewa kipaumbele. Ujerumani imekuwa na jukumu kubwa katika mazungumzo ya kutoa mikopo kati ya wakopeshaji wa kimataifa na nchi za Ulaya zilikabiliwa na mgogoro wa kifedha. …………..
Posted on: Sun, 21 Jul 2013 03:40:47 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015