WAKULIMA MORO WAMEANZA KUNUFAIKA KWA KUPEWA ZANA ZA - TopicsExpress



          

WAKULIMA MORO WAMEANZA KUNUFAIKA KWA KUPEWA ZANA ZA KILIMO. WAKULIMA Mkoani Morogoro wameanza kunufaika na sera ya uwekezaji katika kilimo kwa kurahisishiwa dhana za kilimo zikiwemo pikipiki zinazohimili mazingira ya kilimo Tanzania kupitia kampuni ya Mpembwa General Business kwa ushirikiano na kampuni ya Kichina ya G.S.Group. Mkurugenzi wa Kampuni ya Kizalendo Mpembwa General Business Ltd,Peter Mpembwa asema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya waklima kunufaika na zana hizo. Mkurugenzi huyo amesema kuwa pikipiki hizo zinauwezo wa kuhimili tope na mazingira ya milima na mabonde na hivyo kumrahisishia mkulima kufika maeneo yote ya mashamba bila kukwama. Aidha amesema kuwa pikipiki hizo zitamsaidia mkulima kumwondoa katika wimbi la umaskini kutokana na kutumia mafuta kidogo. Kampuni hiyo pia imeandaa mkakati wa kuhakikisha inauza na kukopesha zana za kilimo kama matrekta ya kupanda na kuvunia mpunga, mbegu za muda mfupi za mahindi na mpunga kwa siku za usoni. Kwa mujibu wa kiongozi huyo,wanatarajia kuuza mbolea za kupandia na kukuzia pamoja na zana zingine za kilimo lengo likiwa ni kumsaidia mkulima kulima kilimo chenye tija na kuondokana na umaskini.
Posted on: Thu, 14 Nov 2013 08:18:49 +0000

Trending Topics



f="http://www.topicsexpress.com/If-youre-looking-for-a-good-gift-for-the-Anglophile-in-your-life-topic-10152913997478033">If youre looking for a good gift for the Anglophile in your life,
Usually the airlines allow international travellers with 2 bags of
U buy Blackberry Q10 for ur girl,another guy pays bis for her dat
So kevin love is with the cavs offically. Wow... So.. umm...
God is my strength and power: He makes my way perfect. Dear
To Bashorun Gaa of Ekitiland (Jogunomi2), Kayode Fayemi and his

© 2015