Wafanyakazi 1,076 watimuliwa Tazara Wafanyakazi 1,076 wa Mamlaka - TopicsExpress



          

Wafanyakazi 1,076 watimuliwa Tazara Wafanyakazi 1,076 wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) upande wa Tanzania wamefukuzwa kazi kutokana na kufanya mgomo usio halali wa siku nne na hivyo kuisababisha mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 600,000 (Sh. milioni 972). Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara, Ronald Phiri, alitangaza jana jioni kufukuzwa kazi wafanyakazi hao wakati akizungumza na waandishi wa habari. Phiri alisema amelazimika kuchukua uamuzi huo kutokana na Tazara kupata hasara ya Dola za Marekani 150,000 kwa siku sawa na Dola 600,000 kwa siku nne walizogoma. Alisema wafanyakazi waliofukuzwa kazi ni wa upande wa Tanzania tu ambao kutoka makao makuu ya Tazara idadi yao ni 826, Mkoa wa Dar es Salaam 120, Mkoa wa Mbeya 53, stesheni ya Kongolo Quarry ni 63 na idara ya Ujenzi ni watano. “Wafanyakazi waliogoma ni upande wa Tanzania tu, lakini wa Zambia hawakugoma, watapewa barua rasmi za kufukuzwa kazi lei,” alisema Phiri ambaye ni raia wa Zambia. Kutokana na kufukuzwa kazi wafanyakazi 1,076, watabakia wafanyakazi 312 kwa kuwa mamlaka ina jumla ya wafanyakazi 1,388. Wafanyakazi hao walianza mgomo tangu wiki iliyopita wakishinikiza kulipwa malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu wanayodai tangu Mei mwaka huu.
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 08:29:26 +0000

Trending Topics




© 2015