Wandugu wa Bondo duniani. Ninafuraha yakuwajulisha kama leo - TopicsExpress



          

Wandugu wa Bondo duniani. Ninafuraha yakuwajulisha kama leo nimepokea habari rasmi kutoka kamati ya ujenzi wa Centre Pediatrique ya kazimia kwamba tayari wameunguza 50,000 matofali yaani briques kama phase ya kwanza ya mchango wao kama walivyo haidi participation locale yao. Kama munavyo helewa kinacho hitajika sasa ni kuanza kazi za ujenzi wa nyumba ya kwanza. Tayari tulinunua manjanja 154. Manjanja hiyo hilipatika kwa michango ya wandugu wa Danmark US$945, Ndugu yetu mmoja Mbondo anaye ishi Allemagne alitoa US$ 100 yaani manjanja 10 na Harare, Zimbabwe Ndugu Joseph Boomenyo na jamaa lake walitoa US$ 500 yaani manjanja 50. Jumla ikawa manjanja 154. Sasa tunahitaji michango na msaada wakununua cement saki 175 ili waanze kujenga nyumba ya kwanza. Unaweza kutoa saki kumi, tano, au moja kulingana na uwezo wako. Saki moja ya cement ni US$ 22 pamoja na transport mpaka Kazimia. Tunahitaji saki 175 kwa kila nyumba. Hivi tutaanza kujenga nyumba ya kwanza. Kupunguza garama za transport, tungependelea cement na manjanja hipelekwe Kazimia pamoja maana manja bado yako Uvira yanangojea mzigo wote huenee pamoja na cement ya angalau nyumba moja yaani 175 ya cement. Kwaimani, pamoja na ushirika wakila Mbondo, tunajua Mungu ametupa ushindi tayari katika projet pilote hii ili kuboresha maendeleo ya jamii katika territoire ya Fizi. Kama unavyo faamu jambo hili sio siri maana hata katika Biblia kuna watu kama vile Nehemia, walijitolea pamoja na nguvu za Mungu, walifanyikiwa kujenga upya ukuta wa Yerusalemu na kuleta uomusho au maendeleo inchini kwao. Wewe na Mimi tuna mzigo huo tuungane katika ujenzi wa Territoire ya Fizi kwa njia na maono na vitendo. Nakuimiza ndugu mbondo usome kitabu cha Nehemia na utahelewa mambo haya. Tayari nimekwisha kupokea hitaji zingine kutoka wa Bondo wa Hibende, Lulenge, Mtambala na mboko. Yote hii tunaweza kuyafanyia kazi kwa pamoja na kwa neema ya Mungu tutaweza kuleta mabadiliko katika Territoire ya Fizi. Uomoja ni nguvu.Maendeleo ya kudumu huletwa na watu kwa Nguvu na neema ya Mungu tunaweza na tutaweza. Mungu wa mbingu atatuwezesha na kutushindia Nehemia 2:20.Tuma mchango wako
Posted on: Wed, 02 Oct 2013 09:41:32 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015