YALIYO JIRI NDANI YA MYAKA 3 NDANI YA SEREKALI INAONGONZWA NA - TopicsExpress



          

YALIYO JIRI NDANI YA MYAKA 3 NDANI YA SEREKALI INAONGONZWA NA CHAMA CNDD FDD. Baada yakusikiya yaliyo semwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ndani ya myaka 3 imepita akiwa madarakani, chama FLP kinapenda kuwafikishiya haya ya fwatayo. 1- FLP ingependeleya kusikiya Rais Nkurunziza akisema wanasheherekeya myaka 8 imepita kwakucaguliwa kuwa Rais wa Burundi, tofauti nalivyo sema ni myaka 3 wanayo sheherekeya. FLP tukicukuliya hiyo hiyo myaka 3 Rais amedayi kuwa Burundi usalama ulikuwa mzuri, tunaona kama siyo kweli mana mnamo myaka hiyo 3 Burundi iligubikwa na mauwaji yasiyo na mfano. Kuanziya 2010 hadi 2012 watu zaidi ya 483 waliuwawa, 429 walijeruhiwa. Watu 24 waliuwawa na jeshi la taifa Watu 36 waliuwawa na polisi la taifa. Watu 69 waliuwawa na idara ya upelelezi ( Documentation ). Watu 158 walidaiwa kuwawa namajambazi, wengine 169 walikutwa wamefariki sehem mbali mbali biza kujulikana walowauwa. Ndani ya hutuba ya Rais Nkurunziza hakusema kuhusu wala rushwa, lakini Burundi hadi leo inachukuwa nafasi ya kwanza kwakula rushwa ndani ya inchi zimeunda shirika la Est Africa, mwaka 2011 Burundi ilikuwa na asilimiya 36.7% zawatu wanakula rushwa. Ndani ya myaka 3 imepita umasikini Burundi umezidi kipimo, watu wanaishi kwa utapiyamlo, ajira hamna, mbaya zaidi ndani ya myaka hiyo hiyo Soko kuu la mjini Bujumbura limeunguwa wakati walokuwa wanastahili kulizima wakishangiliya linavyo unguwa. Kwahayo chama FLP kimeonyesha hapo , tunaona kama utawala wa chama CNDD FDD umefeli kuleta ubora wamaisha yawanaichi, kuhimarisha usalama wa taifa, na tunamtaka Rais Nkurunziza kujiuzulu haraka iwezekanavyo. Chama FLP tunaona baaba ya Rais Nkurunziza kujiuzuli Burundi iwepo serekali ya mpito ambayo itandaa ucaguzi wa mwaka 2015 kwa usalama piya serekali hiyo iweze kuinuwa ubora wa maisha yawana inchi waweze kwenda kucaguwa wakiwa na hafweni ya maisha. Piya iweze kurekebesha mazingira mazuri na mataifa mengine, kitu ambaco serekali yasasa kimeishinda kutekeleza. Kwaniyaba ya Chama FLP Ndayishimiye Atibu Gaspard Mwenyekiti wa chama FLP
Posted on: Wed, 28 Aug 2013 16:35:25 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015