"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba v "Hallow - TopicsExpress



          

"YANI MI NI ZAIDI YA MSHUMAA" Namba v "Hallow nani mwenzangu.......?"Niliuliza baada ya kuipokea simu ile "Mimi Juma,,mambo vipi lakini"Juma alijitambulisha kisha akanisalimia "Safi ndugu yangu,,mbona umetumia namba ngeni?"Nilimuuliza huku nikipunguza hofu "Hii namba ya shemeji yako,,simu yangu haina ata hela ya kubip"Juma aliongea "Enhee nakusikiliza ndugu yangu"Nilimwambia Juma huku nikianza kutembea kuelekea tena sebleni kwa ajili ya kuendelea kunywa chai yangu "Bwana kuna taksi haina dereva so kama unaweza kesho uje uichukue ili uzugiezugie wakati unaendelea kuafuta kazi"Juma aliniambia "Bwana kweli ndugu yangu......?"Nilimuuliza vizuri Juma mana sikuamini kabisa nilichokisikia "Kweli ndugu yangu,,kuna dereva mmoja ameiacha,,,nimeona si vibaya kama nikikushtua ndugu yangu"Juma aliongea akionekana kuwa na uhakika "Nashukuru sana Juma,,kesho mapema sana nitakuwa hapo ili unikabidhi hiyo gari"Niliongea nikiwa na furaha kifupi nilifurahia sana!! Nilimaliza maongezi na Juma nikiwa na furaha ya ajabu,,nikanywa chai haraka kisha nikaenda zangu chumbani kwa ajili ya usafi wa cumba changu!! *********** Usiku nilimueleza mama taarifa ile,,mama alionekana kutofurahishwa kabisa na mi kuwa dereva taksi "Yani mwanangu una degree ya uchumi leo hii ukawe taksi driver?"Mama aliniuliza "Nikweli mama kitu ambacho kinashangaza lakini ni afadhali iwe hivyo kuliko kuendelea kukaa bila kazi"Nilimwambia mama kwa sauti ya unyonge "Nimehangaika sana kutafuta kazi na we ukiniona,,imefikia hatua natembea kwa miguu umbali mrefu sababu ya kukosa ata mia mbli tu ya nauli,,ni afadhali nipoteze muda kwa kupata vimia mbilimbili ili ata wewe nisikusumbue tena hizi hela za vocha"Nilimwambia mama maneno yaliyoonekan kuanza kumuingia kichwani kwake "Aya mwanangu ila tu usiache kuendelea kutafuta kazi"Mama aliniambia akionekana kuridhika kabisa na mi kufanya kazi ile "Sawa mama nitaendelea kutafuta kazi wala sitaacha"Nilimjibu mama huku moyoni nikisema kuwa sitahangaika tena kutafuta kazi sehemu yoyote ile!! Jumapili na mapema nilikuwa nimeshafika anapoishi Juma,,kweli nikakuta taksi mbili zimepaki nje ya nyumba anayoishi "Afadhali umewahi ndugu yangu....."Juma aliongea akionekana na yeye kuwa na haraka kidogo "Gari ndo hii hapa nadhani unaiona mwenyewe"Juma aliongea akinionyesha ile taksi aliyotakiwa kunipa "Nadhani mwenyewe unaelewa mazingira ya kazi za taksi kwa kuwa muda mwingi upo na mimi na ata bosi wa hizi gari najua unamfahamu vizuri"Juma aliniambia huku akiniangalia usoni "Hakikisha unaitunza vizuri hii gari na kila siku uniletee elfu ishirini na tano kwa ajili ya tajiri"Juma aliniambia wakati ananikabidhi funguo za gari "Leo jumapili huwa hatufanyi kazi kwahiyo nafikili utaanza kesho kuleta kipande cha tajiri,,na hapo ilipo mafuta ni full tank,,mwisho wa mwezi ukifika mshahara wako wa elfu sabini unapata bila matatizo"Juma alimaliza kunipa maelekezo "Sawa ndugu yangu nimekuelewa,,nashukuru sana kwa msaad wako"Nilimshukuru Juma kisha nikaingia ndani ya gari ile na safari ya kuelekea Tabata kwa yule mrembo ikaanza!! Nilitumia dakika thelathini tu kufika nje ya nyumba aliyokuwa akiishi yule mrembo,,nilipofika pale nilimkuta yule mdogo wake amesimama nje akionekana kumsubiri mtu ili waondoke "Karibu sana anco.........."Mdogo wake aliyeonekana kunikumbuka vizuri alinikaribisha kwa furaha "Asante sana,,habari za siku?"Nilimsalimia mdogo wake yule mrembo "Salama,,karibu ukae........."Yule binti alinikaribisha kwenye kiti kilichokuwa pembeni yake "Mi sio mkaaji kabisa,,vipi dada yako yupo au ametoka?"Nilimuuliza yule binti "Dada yupo anakuja sasa hivi......."Yule binti alinijibu,ghafla mlango ukafunguliwa sura ya mrembo niliyemfuata ilijitokeza "Duuh kweli huyu mtoto ameumbika jamani"Niliwaza mwenyewe moyoni baada ya kuiona miguu mizuri ya mrembo yule aliyekuwa amevaa kimini cheusi pamoja na blauzi nyekundu huku miguuni akia amevaa skuna nyekundu "Enhee jamani karibu anco........."Mrembo alinikaribisha kwa furaha aliponiona "Asante sana,,safari ya wapi tena saa hizi?"Niliuliza baada ya kuona wapo kimtoko zaidi "Tunaenda kwa shangazi maeneo ya mbezi"Yule mrembo alinijibu huku akiniangalia usoni "Mbona kimya sana tangu siku ile.?"Nilimuuliza yule dada "Nilipoteza namba zako"Alinijibu akionekana kuwa muwongo mana alianza kucheka mwenyewe "Naomba niwasindikize basi huko mbezi mnapokwenda"Nilimwambia mrembo yule aliyeonekana kuwa mtu wa masikhara sana "Sawa hakuna tatizo......"Mrembo yule alikubali,,nikawafungulia milango ya gari ila huyu mrembo wa moyo wangu alikuwa amekaa siti ya mbele kabisa "Humu humu kwenye gari ntamueleza yote yanayonisumbua moyoni"Niliwaza wakati nawasha gari kwa ajili ya safari ya mbezi bila kujali kama ndo kwanza nimekabidhiwa gari lisaa limoja tu lililoisha!! ********** Itaendelea............... Nawatakieni Jumapili Njema Wapendwa Comment Na Like Nyingi Zinahitajika Kabla Ya Namba vi By #Hajrat_Classic_Mudboy
Posted on: Sun, 25 Aug 2013 06:12:48 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015