Yanga: Tutaipiga Simba 3-0 J`Pili..........(yetu - TopicsExpress



          

Yanga: Tutaipiga Simba 3-0 J`Pili..........(yetu macho.)...... -------------------------------- Ofisa habari wa Yanga,Baraka Kizuguto(kulia)akizungumza na mmoja wa wanachama Yanga wakati wa mkutano wa viogozi wa matawi,Baraza la Wazee wa Yanga na kamati ya utendaji ya klabu hiyo kwa ajili ya kupanga mikakati ya kumuua Mnyama Simba kwenye makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam. Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga wamesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji, Baraza la Wazee na matawi ya Yanga ya jiji la Dar es Salaam kilichofanyika kwenye ofisi za makao makuu ya klabu hiyo jijini jana, msemaji wa matawi hayo, Bakili Makele alisema mipango ya kumuua mnyama imeshakamilika na wameshahakikishiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 katika mchezo huo mgumu dhidi ya vinara wa ligi. tumekutana matawi yote ya Yanga ya Dar es Salaam, Baraza la Wazee na Kamati ya Utendaji kujadili namna ya kumuua Mnyama. Tumepokea taarifa kutoka kwenye Kamati ya Utendaji, Sekretarieti na Baraza la Wazee la Yanga kwamba mipango yote inakwenda vizuri, hakuna matatizo kwenye timu na hatuna majeruhi hata mmoja. Tunapiga magoli matatu Jumapili, alisema Makele. Tunaomba nidhamu kwa wanachama na mashabiki wa Yanga siku hiyo. Tunaomba pia refa na wasaidizi wake siku hiyo wawe makini maana wapinzani wetu mechi zao ni za penalti. Kila mechi wachezaji wao wanajiangusha na kupewa penalti zisizo halali, alisema zaidi Makele, ambaye pia ni kiongozi wa Tawi la Yanga la Temeke.
Posted on: Sat, 19 Oct 2013 04:56:24 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015