Zitto Z Kabwe Kodi ya Kadi za simu (simcard tax) ni kama vile Hut - TopicsExpress



          

Zitto Z Kabwe Kodi ya Kadi za simu (simcard tax) ni kama vile Hut Tax ambayo wakoloni walianzisha na babu zetu kukataa kwa kupigana vita. Poll tax pia wazee wetu waliikataa. Wabunge tumepitisha kodi hii kwa sababu sisi tunazo za kulipa. Kati ya watanzania 28m wenye simu, 8m wanatumia chini ya tshs 1000 kwa mwezi kwenye simu zao. Hii Itakula kwa kampuni za simu kwa Serikali inataka 1000 yao tu. Kwa hiyo kampuni za simu zitaongeza gharama za simu uli kufidia hilo. Kwa hiyo Itakula kwetu. Badala ya Serikali kutoza kodi makampuni (corporate tax) wao wamekimbilia kwa wanyonge. Tigo na airtel zimesajiliwa offshore (Luxembourg na Netherlands respectively), Zantel Dubai. VodaCom angalau wamesajiliwa hapa nchini lakini hawalipi kodi kabisa. Nina maana kodi ya mapato na sio kodi kama ushuru wa bidhaa na VAT ambazo mlipaji ni Mwananchi. 6 hours ago Like · 249 Comments · Share 210 people like this.
Posted on: Sat, 06 Jul 2013 10:35:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015