katika moring bell siku ya leo utapata mengi zaidi ni pamoja - TopicsExpress



          

katika moring bell siku ya leo utapata mengi zaidi ni pamoja na Mgogoro wa ardhi kati ya shule ya sekondari Ndugu iliyopo katika mtaa wa Hasamba Kata ya Vwawa wilayani Mbozi dhidi ya waziri mstaafu wa ardhi Gidion Cheyo umemalizika juzi baada ya pande zote mbili kukutana na kufikia suluhu katika mkutano uliofanyika shuleni hapo. HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya imepata hasara ya mamilioni ya fedha kutokana na kukosa kumbukumbu za vyanzo vyake vya mapato, zikiwamo nyumba inazomiliki kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwatambua wapangaji wake kisheria. MWAMKO mdogo wa kielimu kwa wazazi wilayani Kyela, Mbeya ndiyo chanzo cha kusababisha wilaya hiyo kushika nafasi ya kwanza kwa kufanya vibaya kimkoa katika nyanja ya elimu nchini. WAKAZI wa Wilaya ya Ileje, mkoani Mbeya wanaoishi jijini Dar es Salaam, wameitaka serikali irudie upya mapendekezo ya kutaka makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe kuwa Mkwajuni katika Wilaya ya Chunya. Mgogoro wa ardhi kati ya shule ya sekondari Ndugu iliyopo katika mtaa wa Hasamba Kata ya Vwawa wilayani Mbozi dhidi ya waziri mstaafu wa ardhi Gidion Cheyo umemalizika juzi baada ya pande zote mbili kukutana na kufikia suluhu katika mkutano uliofanyika shuleni hapo. Mgogoro ambao umedumu kwa muda wa miaka kumi ulifikia suluhisho kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya na Mbunge wa Mbozi Godfrey Zambi kuwakutanisha wananchi wa Hasamba na waziri mstaafu wa ardhi Gidion cheyo ambaye ndiye alikuwa anamiliki eneo hilo ambalo lilikuwa na utata kwa wananchi. Akizungumza katika mkutano huo waziri mstaafu Gidion Cheyo amesema kuwa yeye hana nia mbaya na wananchi wa Hasamba na Mbozi kwa ujumla hivyo ameamua kuwaachia eneo hilo lenye ukubwa wa ekari nne kwa ajili ya maendeleo ya shule ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu na madarasa. Amesema mawasiliano mabaya kati ya msimamizi wake katika maeneo hayo ndio yaliyosababisha kuonyesha kuwa yeye anang’ang’ania eneo hilo. Aidha Cheyo alimtaka mtendaji wa Kata ya Vwawa Joel Kaminyoge kushirikiana na kaimu mkuu wa ardhi Moses Kibona na kufuata taratibu za kisheria ili eneo hilo liweze kurudi kwa wananchi. Joel Kaminyoge mtendaji wa Kata ya Vwawa amewaahidi wananchi kuwa atafuatilia haraka iwezekanavyo ili kutengua na kubadilisha hati ya eneo hilo ili lirudishwe kwa wananchi na liendelee kutumika katika maendeleo ya shule ya sekondari Ndugu. Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi Godfrey Zambi alimshukuru Gidion Cheyo kwa kusikia kilio cha wananchi wa Hasamba na kuwaachia eneo hilo pamoja na miti aliyopanda bila kuppelekana mahakamani. HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Mbeya imepata hasara ya mamilioni ya fedha kutokana na kukosa kumbukumbu za vyanzo vyake vya mapato, zikiwamo nyumba inazomiliki kwa zaidi ya miaka 20 bila kuwatambua wapangaji wake kisheria. Nyumba hizo tatu ambazo ziko katikati ya mji wa Vwawa wilayani hapa kwa sasa zinatumika kama nyumba za biashara ya kupangisha wageni ‘guest house’, baa na ofisi, ambapo moja ni ofisi ya Ushirika wa Umoja wa Wanawake na nyingine ni ya Tanganyika Farmers Association ( TFA). Hoja ya upotevu huo wa mapato imeibuliwa na Diwani wa Ihanda, Joel Kasebele na baadaye kuungwa mkono na madiwani wengine kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa Halamshauri ya Wilaya ya Mbozi. Diwani Kasebele alimuuliza Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo ambaye ndiye katibu wa kikao hicho juu ya mustakabali wa nyumba hizo zinazojulikana kwa majina ya TFA, Selfina na MDC (Mbozi District Council) ambazo zinadaiwa kumilikiwa na halmashauri hiyo tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980 ulipoanzishwa mfumo wa serikali za mitaa. Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Levison Chilewa, alikiri kuwapo kwa nyumba hizo pamoja na nyingine zilizokuwa zikimilikiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na baadaye kuiuzia halmashauri hiyo. Pia amekiri kuwapo kwa wapangaji, lakini haijulikani walikodishwa na nani na ni kwa kipindi gani (miaka mingapi) hadi sasa. Hata hivyo, amejitetea kuwa yeye na wataalamu wengi wa halmashauri hiyo ni wageni, hivyo hawakukuta kumbukumbu zozote ofisini kutoka kwa waliowarithi. Kutokana na hali hiyo, ameliomba baraza hilo kumpatia muda kulifuatilia jambo hilo na kuahidi kulitolea maelezo katika kikao kijacho. MWAMKO mdogo wa kielimu kwa wazazi wilayani Kyela, Mbeya ndiyo chanzo cha kusababisha wilaya hiyo kushika nafasi ya kwanza kwa kufanya vibaya kimkoa katika nyanja ya elimu nchini. Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, amebainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo cha Ufundi na Biashara Kyela (Kyela Polytechnic College) yaliyofanyika chuoni hapo. Amesema Wilaya ya Kyela ni miongoni mwa wilaya 40 ambazo zimekuwa zinafanya vibaya katika elimu na kwamba ni wilaya ambayo inashika nafasi ya kwanza kimkoa. Amesema kutokana na mwamko mdogo wa wazazi kielimu ndiyo maana chuo hicho kimekuwa na wanafunzi wachache tofauti na mikoa mingine ambayo imekuwa na vyuo. “Ni heri niache ubunge wangu kuliko kuangalia suala baya kama hili wilayani Kyela likiachwa kama ilivyo kwa kuwa hii ni aibu kwetu sote hasa wakazi wa wilaya hii na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla,” alisema Mulugo. Ameongeza kuwa kutokana na tatizo hilo, serikali imeiingiza wilaya hiyo kuwa miongoni mwa wilaya zilizopewa kipaumbele katika utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now), ili kuongeza ufanisi katika uchapaji kazi. Amesema kutokana na mpango huo ni lazima viongozi wawajibike ipasavyo katika kusimamia suala hilo na kusema ikiwezekana walimu wakuu na maofisa elimu wawajibishwe iwapo watathibitika kufanya uzembe katika jambo hili. Mkuu wa chuo hicho, Dk. Salatiel Mwakyambiki, amesema Kyela inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya biashara ndogondogo na matumizi ya simu kwa wanafunzi wawapo darasani ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo yao. Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kujikita katika elimu kwa kujiunga na vyuo, ili kuondokana na aibu ya kuwa wa mwisho kimkoa katika sekta ya elimu. WAKAZI wa Wilaya ya Ileje, mkoani Mbeya wanaoishi jijini Dar es Salaam, wameitaka serikali irudie upya mapendekezo ya kutaka makao makuu ya mkoa mpya wa Songwe kuwa Mkwajuni katika Wilaya ya Chunya. Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa wakazi hao, Janes Musokwa, alisema wao wanaelewa uanzishwaji wa mkoa mpya ni kwa ajili ya kuleta huduma karibu na wananchi, lakini katika mchakato huo huduma zitasogezwa mbali na wananchi kwa kilometa 100 zaidi. Amesema kwa umbali huo wanalazimika kuunga mkono mapendekezo ya wilaya ya Momba na Mbozi kutaka makao makuu ya mkoa mpya yawe Vwawa, Mbozi. Musokwa amesema kwa sasa wakazi wa Ileje wanalazimika kutumia kilometa 130 kutoka Ileje hadi Mbeya mjini lakini watalazimika kwenda kilometa 230 kufika Mkwajuni, na itamlazimu mwananchi wa Ileje kupita mkoa wa Mbeya kufika makao makuu ya mkoa wa Songwe Amesema kama itashindikana kurudiwa au kubadilisha makao makuu ya mkoa mpya ni afadhali wabaki kuwa sehemu ya mkoa wa Mbeya. JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya SMG, risasi 20 na bastola kutoka Slovakia ikiwa na ganda moja, zikiwa katika gari. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 2, mwaka huu, majira ya saa tatu katika eneo la Kiparang’anda lililopo Barabara ya Kilwa, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani. Amesema siku ya tukio askari F. 3634 PC Sihoja alikamata silaha hizo zikiwa ndani ya gari T 229 AZE Ford Hiace, pamoja na watu wanne. Kamanda Matei alisema silaha hizo zimefutwa namba na kwamba gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Sunday Ngonyani (35) mfanyabiashara wa Mtoni Mtongani, Dar es Salaam. Amewataja watuhumiwa wengine waliokamatwa wakiwa ndani ya gari hilo kuwa ni Athumani Ally (38) mkazi wa Kongowe, Dar es Saalam, Nasiru Omari Mohamed (39) mkazi wa Mbande na Peter Mathias (40) mkazi wa Mtoni Mtongani, Dar es Salaam. Mbali ya kukamatwa na silaha hizo, watuhumiwa hao pia walikutwa na kofia za kufunika uso, ambazo bado haijajulikana kazi waliyokuwa wakifanyia. Kamanda Matei amesema kwa sasa watuhumiwa hao wako kwenye mahojiano na Polisi. ambatana nami Richie flavour pamoja DAZZLE KWAITO
Posted on: Tue, 06 Aug 2013 04:26:45 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015