A DIAMOND CITY. CHARLES J LIGONJA ( Na fikra mpauko) Sipendi - TopicsExpress



          

A DIAMOND CITY. CHARLES J LIGONJA ( Na fikra mpauko) Sipendi kusikia kitu siasa katika maisha yangu,siasa mchezo mchafu sana,majungu,fitina n uzandiki ni sehemu ya siasa za nchi ya NATAZANI,kwanini niingie huku kama mm sio muumin wa hayo mambo,Mungu nisaidie nisiwe mwanasiasa. Nikiwa njian kutoka mjini Nzega mkoani Tabora siku ya 27/9/2013 kuelekea mjini Kahama ikiwa kama siku nne zimepita tangu nirejee toka Mwanza nilikoambatana na familia yangu,niliingia Kahama na lengo likiwa niunganishe moja kwa moja mpaka Kigoma lakini kwa bahati mbya nikakosa gari la kunifikisha huko,nikaamua kutafuta guest na kulipia chumba ili nilale hapo na asubuhi niendelee na safari yangu. Kati ya majiji niliyofiki hapa Tanzania nimejikuta naipenda sana Mwanza kutokana na hali ya hewa lakini usafi pia lakini hata Kahama ni mji mzuri na hilo linatokana na mabadliko ya kiuchum katik huo mji,kila mtu yuko busy kuhakikisha anatafuta chake ingawa wale ambao kufanya kazi sio hulka yao au wategaji nao wapo wamekalia kulalamika tu na maisha yanawapiga kweli,hao siwajali sana kwasababu inawezekani hawajajua wapi pa kuanzia au nini wafanye ila ipo siku watang’amua kwamba lazima wafanye kazi kwani asiyefanya kazi na asile. ***** Nikiwa guest mara nikipata wazo na kuona ni bora nikaandika na kama itatokea mmoja akasoma na kufikisha ujumbe wangu kwa BABA YETU MKUBWA na kufanyiwa kazi basi nitakuwa na amani sana.Wazo gumu sana lakini kama kuna nia ya dhati basi hakuna ugumu katika kuhakikisha linatekelezwa na anaweza akaanza yeye (phase one) hata kwa kuweka mchoro tu na badae akija BABA MKUBWA mwingine basi utekelezaji hatua ya kwanza ungeanza . BABA YETU MKUBWA akifanya hivyo basi ntaiona KAHAMA kwenye sayari nyingine,natamani watoto na wajukuu wetu waje na kujivunia uwepo wetu hapa duniani,wakija waseme kweli babu na baba zetu au bibi zetu walikuwa na akili sana kwani wametengeneza mji mkubwa na wa kisasa,mji ambao kila mtu anatamani kuishi,mji ulio na miundombinu ya kila aina tena ya kisasa na bora,ukianza na barabara,maji safi na salama,hospitali zilizosheheni wataalam na huduma za kila aina zinapatikana hapo,nyumba bora zilizojengwa katika mpangilio ulio sahihi,vumbi likitokea basi bahati mbaya,Kahama iwe kijani,hakuna mafua,homa,njaa n.k hivi kwa ule utajiri ulioko pale wanapochimba yale maudongo haiwezekani kuwa na A DIAMOND CITY na kuwa mji wa mfano Afrika?INAWEZEKANA. Suala la ulinzi lisiwepo kwani wezi/wizi hautakuwepo,unalala mlango wazi na marufuku kujenga nyumba na kuweka geti la chuma , lanini wakati hakuna wezi,kila mtu anajitosheleza,kodi ya nyumba kwa mwezi 1000/= na ukiingia ndani unakuta kila kitu,ukarimu unarudi na kuwe wa kisasa zaidi kwani ukifika kwa mtu unaingia jikoni na kupima chakula ukipendacho na kula (******** huo wazimu sasa hahahahaha!!!) na kama unatembea mtaani na kukuta pesa imeangushwa basi iokote na kuipeleka polisi na polisi watangaze kwenye vyombo vya habariili aliyepoteza hiyo pesa aje achukue au apige simu na jeshi la polisi limpelekee pesa yake nyumbani. Watu waheshimiane kuanzia mtoto mpaka mtu mzima,kusiwe na matabaka yasiyo na umuhimu kwani matabaka yanahasara zake,hakuna mtu kumuonea wivu mwenzake kwasababu kama nyumba zote zinafanana,gari pia,dawa wote mnatumia za aina moja,sio huyu panadol ya laki moja huyu ya shilingi kumi,viongozi watibiwe Kahama ,muda wa kazi nao lazima ufanane kwani ingawa maisha yatakuwa safi lakini kufanya kazi usiku na mchana na hakuna kupumzika labda sikukuu ya Idd na Krismass yani jumatatu hadi jumapili kazi tu saa ishirini na nne,mavazi nayo jumatatu wote suti,jumanne t-shirt na jeans,jumatano wote mnavaa nguo za vitenge,alhamis kanga,ijumaa mitandio,jumamosi boksa na kwenda kushinda beach(**********hahahahahaha****) na jumapili siku ya kuchoma nyama hivyo mtavaa eploni juu ya hizo boksa,mtapendeza sana!! Leo hii Kahama ina majengo mazuri,watu wamefanya uwekezaji mkubwa sana lakini changamoto nazo ziko nyingi sana,barabara bado mbovu,mitaa haieleweki,mjini kuna nyumba za ajabu bado ambazo kwenye hiyo DIAMOND CITY serikali lazima ivunje na kufidia hao watu na kujenga nyumba za kisasa na kuwapangisha kwa kodi ndogo sh 1000 kwa chumba yaani apartment yenye vyumba vitatu,choo,jiko,sehemu ya kusomea (maktaba ya ndani) sawa na bure,hapo naamini vijana wanaofikiri kwenda kufanya kazi kwenye miji mikubwa kama Dar es salaam na kuishia kulala kwenye baraza za maduka ya Wachaga na Wahindi kule kariakoo basi hawatathubutu kwenda huko kwani ajira nazo zitakuwa za mikataba,miaka mitano unaachia ofisi na kuingia mwingine sio leo kuna watu wako ofisini zaidi ya miaka arobaini na kibaya zaidi wengine wezi na wala rushwa wakubwa,wapo na mitumbo yao,ah!!!! ***** Kabla sijamaliza kuandika mara likaja wazo la kutamani kula matunda na hapo nilivaa ndala za mle chumbani ambazo kutokana na kutoaminiana mmiliki wa guest amezikata ili mteja asije akaondoka nazo , kwenye DIAMOND CITY hakuta kuwa na hofu kama hizo,nilitoka nje kama mita mia mbili hivi na kukuta banda la matunda.niliagiza na kuanza kula matunda baada ya kujihakikishia jamaa katika suala la usafi anakaribia DIAMOND CITY akaniwekea tikiti maji,ndzi,tango,papai,embe na karoti sijui mchanganyiko huo unaitwaje na sina uhakika kama mzuri kiafya,majanga! Nikiwa nimenogewa kula mara kwa mbali niliona msichana mrembo anakuja na nilipotupa macho vizuri alikuwa Tina,jamani Tina aliyesemekana amekufa baada ya ndugu zake kumtuhumu kusababisha kifo cha baba yake kumbe yuko hai na ameweza kupata mkono wa bandia hivyo kama ulikuwa hujui kama alikatwa mkono na vijana wa baba yake basi utajua yuko sawa (usisahau Simulizi yangu itakayokuja kwenye kitabu …..MSAKO) “Tina!” “Charles!” Kila mtu alishangaa kumuona mwenzake mahala pale,alikuja na kunikumbatia kwa nguvu mpaka nikaanza kurudisha zile hisia za mapenzi tuliyokuwa nayo miaka mitano iliyopita. “Mambo Tina!” “Poa,za siku nyingi?” “Unakwenda wapi ?” “Niko njiani kwenda kigoma,nimefikia Rivermark” “Kumbe mambo yako safi,twende” “Poa” Sikuwa na muda wa kuuliza tunaenda wapi zaidi ya kumshika mkono na kwenda nae mpaka kwenye hyo nyumba na kuingia nae mpaka chumbani na tulipofika huko hakuna kingine tulichoanzia zaidi ya kufikia kitandani na kujikumbushia miaka mitatu nyuma.ilipigwa game ya nguvu na baada ya saa kama nne hivi kila mmoja alikuwa hoi,hamu ilikuwa imeisha kilchobaki ilikuwa tamaa tu za miili. Saa sita badae nlikuwa tayari nimepiga raund kama sita hivi na nikiwa kwenye maandalizi ya kuingia bafuni kupiga maji mara simu iliita na nilipopokea alikuwa rafiki yangu ambae aliingia facebook na kukuta status inayoeleza mahali nilipo siku hiyo (Kahama) “Nambie Dawson?” “Uko wapi wewe?” “Rivermark guest” “Poa nakuja sasa hivi,tokeza hapo barabarani basi” nilipotoka alikuwa Dawson akiwa na gari matata BMW ya silver na kutafuta mahali pa kupaki na alipopata sehemu ya kupaki vizuri alifanya hivyo. “Twende ukamsalimie shemeji yako” “Hujaacha tu!” “Kaka kulala guest peke yako hasara yani 50,000/= afu alone,dah!” “Poa twende nikamsalimie wifi yangu” Alipoingia tu alikutana na Tina na kupigwa na butwaa na kunigeukia na kuanza kulia na nilipotaka kujua kulikoni nae Tina alitaka kutoka na kuondoka. “Subiri” “Kuna nini,kama ulipita basi nisamehe maana yake hawa wanawake bwana ngoja tugawane tu” Masikini kumbe haikuwa hivyo,Tina alijulikana kwa jina la TUFE WENGI na hilo lilitokana na kutendwa mara baada ya kuwakimbia ndugu zake,hakuwa na mbele wala nyuma,mwili wake ulikuwa kitega uchumi pekee na katika hilo alipata mzungu mmoja aliyemnunulia huo mkono wa bandia lakini walikuja kuachana baada ya kumfumania na njembe nyingine. “Tina una UKIMWI?” “Umezidi kuparamia,ukome!” “Nini!!!” “Nyoo” ***MWISHO*** ***KUNA WATU WAKO HIVI AKIWA SAFARINI NA IKATOKEA DHARULA YA KUMLAZIMU KULALA NYUMBA YA WAGENI BASI LAZIMA ATAFUTE MWANAMKE..ETI KULALA GUEST PEKE YAKE HASARA*** ***HAYA SASA KIPI HASARA KULALA PEKE YAKO AU KUPATA UKIMWI?***TAKE CARE. JUMAPILI NJEMA Na Charles J Ligonja.
Posted on: Sun, 17 Nov 2013 09:37:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015