BAADA YA MUDA ULIOAMRIWA KUPITA. Wana wa Israel waliambiwa - TopicsExpress



          

BAADA YA MUDA ULIOAMRIWA KUPITA. Wana wa Israel waliambiwa watakaa utumwani muda wa miaka 400 lakini wao walikaa utumwani miaka 430. Tatizo hili hatulioni kwa wana wa Israel pekee yao, mpaka hivi leo wapo watu wengi wa Mungu wanaishi nje ya kusudi la Mungu, kwa sababu muda ulioamriwa ju ya maisha yao ulikuja na hawakujua kuwa huu ndio muda sahihi kwa ajili ya maisha yao, na pia inawezekana hawakuomba katika muda huo na Mungu naye akaamua kunyamaza. Hapa ndipo mtu anaweza kusubiri kwa muda mrefu sana bila kuona majibu yake au matokeo ya yale aliyoyatarajia. Roho Mtakatifu anapokusukuma kuombea jambo fulani na msisitizo ukawa mkubwa wa kulibeba jambo hilo, lakini ukakosa muda wa kuliombea, au wakati mwingine ukaliombea chini ya kiwango, au wakati mwingine uliwapa watu wakubebee na wewe hukuomba ukijua wao wataomba kwa ajili yako; au kwa wakati huo hukujua nini cha kuombea na wewe hukumuuliza Roho Mtakatifu akufunulie maana maandiko yanasema “Msimzimishe Roho”. (1 Wathesalonike 5:19), usipomtii Roho Mtakatifu, huo mzigo utadumu nao kwa muda mfupi halafu utaondoka na inaweza kuleta vikwazo vingine juu ya maisha yako kwa kukosa kumtii Mungu. Jambo ninalotaka ulijue ni hili, huo ndio muda wa Mungu ulioamriwa katika maisha yako ambao ndani yake umebeba kusudi la Mungu, ikiwa hukuomba na huo muda ukapita jua ya kuwa umechelewesha kusudi la Mungu na utaingia gharama kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel; ni muhimu sana kila wakati, siku zote, mahali popote kumtii na kumsikiliza Roho Mtakatifu kwa sababu yeye peke yake ndiye ajuaye kusudi la Mungu lililofichwa ndani ya muda wako (1 Wakorintho 2:11b). Maandiko yanasema “pasipo maono, watu huacha kujizuia”, hii ina maana kuwa Biblia inaturuhusu kuwa na mipango yetu wenyewe ihusuyo maisha yetu ya kila siku na yale ya baadaye; pia maandiko yanena waziwazi ya kuwa, tutumie akili kama ipasavyo, wala tusitende dhambi (1 Wakorintho 15:34) hii ina maana ya kuwa, akili zetu zimepewa kibali cha kufanya maamuzi pamoja na kupanga mipango yetu pasipo kutenda dhambi, lakini Mungu bado atakuwa na deni juu yetu kwa sababu kusudi lake halijatimia katika muda muafaka, alitupa nafasi na tukashindwa kuitumia hivyo hatuwezi kufanikiwa kama Mungu apendavyo kwa sababu tuko nje ya kusudi na mpango wa Mungu. Hakuna mwanadamu aliyezaliwa kwa hasara au kwa bahati mbaya, kila mmoja ameitwa kulitumikia kusudi la ufalme wa Mungu kwa muda maalum ulioamriwa.
Posted on: Thu, 24 Oct 2013 03:27:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015