COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 14.11.2013: (HABARI). Shehena - TopicsExpress



          

COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 14.11.2013: (HABARI). Shehena kubwa ya pembe za tembo ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini imenaswa katika bandari ya Zanzibar huku ikishuhudiwa na mawaziri wa serikali zote mbili wakiongozwa na waziri wa mali asili na utalii Mhe Khamis Kagasheki. Mamlaka ya Maji Visiwani Zanzibar, imesema inafanya kila jitihada kuhakikisha kila aneo ambalo kuna ukosefu wa maji wanafikisha huduma hiyo. Rais Jakaya Kikwete amewaongoza viongozi na Watanzania katika kutoa mkono wa pole kwa familia ya marehemu daktari Edmund Sengondo Mvungi aliyekuwa mjumbe wa tume ya katiba ambae alifariki dunia nchini Afrika kusini alikokuwa akipata matibabu baada ya kuvamiwa na majambazi na kukatwa mapanga nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Jeshi la Syria limepiga hatua kuelekea katika maeneo yanayoshikiliwa na makundi ya Kiislamu katika kijiji cha kaskazini cha Tal Hassel, wakati waasi wa makundi ya Jihad karibu na Aleppo wakitoa wito wa kupata wapiganaji zaidi ili kuzuwia hatua hiyo. Idadi rasmi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino imepanda na kufikia watu 2,344. Baraza la kushughulikia maafa la taifa limetoa tarakimu hizo leo. NCHI za Mexico na Uruguay Jana zilipiga hatua kubwa kutinga Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil Mwaka 2014 baada kushinda Mechi zao za kwanza za Mchujo za Kimataifa. MAONI: +255 772 389889.
Posted on: Thu, 14 Nov 2013 04:01:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015