COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 26.09.2013: (HABARI). Mwenyekiti - TopicsExpress



          

COCOJAMBO ASUBUHI HII: ALHAMIS, 26.09.2013: (HABARI). Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mboe, amesema Muungaano uliopo kati ya Zanzibar na Tanganyika ni kwa maslahi ya viongozi wachache wa Chama cha Mapinduzi. Mshikamano wa baadhi ya vyama vikubwa vya upinzani vya hapa nchini katika kupinga muswada wa marekebisho ya mabadiliko ya katiba 2013 umeingia Zanzibar baada ya vyama hivyo kufanya mkutano wa hadhara kisiwani Zanzibar na kutamka kupinga muswada huo. Kuelekea mtihani wa darasa la saba na kidato cha pili Visiwani Zanzibar, wanafunzi wa Skuli ya Kitope wamesema wanakosa muda wa kujisomea kutokana na kukabiliwa na tatizo la baadhi ya wanafunzi katika Skuli hiyo kupandisha mashetani mara kwa mara wakati masomo yakiendelea. Mkoa wa Mini Mgharibi unakabiliwa na changamoto kubwa ya amani na utulivu kufuatia matukio makubwa ya uvunjifu wa amani kutokea katika Mkoa huo. Tumezungumza na Mwanasaikoloia kutoka Jijini Dar es Salaam, akituelezea namna ya kuweza kuwaresha katika hali ya kawaida waathirika waliokuwemo katika Jengo la WASTEGATE Jijini Nairobi lilipotekwa na magaidi. Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba kiwango na maambukizi ya ugonjwa wa malaria kinapungua kwa kasi ya kuridhisha nchini Tanzania, bado mtoto mmoja anapoteza maisha kwa ugonjwa wa malaria kila dakika moja katika nchi za bara la Afrika. Kenya imeanzisha uchunguzi wa eneo la mikasa, kufuatia shambulizi lililofanywa katika jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi. Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wamewasili jana nchini Syria ili kuendelea na uchunguzi wao kuhusiana na madai ya kufanyika mashambulizi ya gesi ya sumu, wakati Urusi na nchi za Magharibi zikizozana kuhusu namna ya kuziangamiza silaha za sumu za Rais Bashar al-Assad. Idadi ya watu waliothibitishwa kufa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kulikumba eneo la kusini magharibi mwa Pakistan imepanda na kufika 328 MAONI: +255 772389889.
Posted on: Thu, 26 Sep 2013 02:49:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015