FISTULA Tafsiri fupi ya neno Fistula ni tundu ambalo linapitisha - TopicsExpress



          

FISTULA Tafsiri fupi ya neno Fistula ni tundu ambalo linapitisha au linavujisha kitu. Katika ya uzazi kuna aina mbili za Fistula. 1.Vesco Vaginal Fistula(VVF) Ni kutoka mkojo katika tundu ya uke(uzazi) badala ya tundu ya mkojo bila ya kujizuia.Yaani unakuwa hauna uwezo wa kudhibiti utokaji wa mkojo. 2.Rectal Vaginl Fistula(RVF) Ni kutoka haja kubwa katika uke badala ya sehemu ya kawaida.Pia inatoka bila yakuwa na uwezo wa kujizuia. Kwa hakika haya ni matatizo makubwa yanayowakabili mama zetu,wake zetu na dada zetu.Ambayo yanampekelea kujitenga au kutengwa kutokana harufu kali ya choo kubwa au ndogo inayomtoka. SABABU YA FISTULA. Sababu zinapelekea aina hizi Fistula ni: 1.Mama mjamzito wakati wa uchungu wa kujifungua akipatwa na Uchungu Pingamizi(Obstructed Labour) hali ya kibofu kimejaa mkojo na mtoto anashindwa kupita kuna pelekea msuguano kati ya kuta laini na nyembamba za kibofu cha mkojo na kusababisha tundu(fistula) katika kibofu na mkojo kuvuja kuelekea katika uke.Hivyo hivyo kwa RVF. 2.Pia Fistula inaweza kusababishwa na upasuaji mkubwa hasa ya kujifungua(CS) au upasuaji wowote unaohusu viungo vya uzazi kwa bahati mbaya wakapasua au kutoboa kibofu cha mkojo au rectum. DALILI Ni kutokwa na haja kubwa au ndogo katika uke TIBA Fistula inatibika na kwa sasa tiba inatolewa bila malipo katika vituo vilivyoteuliwa kutoa huduma hiyo. Je una mtu mwenye tatizo la fistula piga namba zifuatazo ili akatibiwe. 0752 678 263(CCBRT) 0765 770 770
Posted on: Wed, 31 Jul 2013 02:11:10 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015