HAKUNA UTAJIRI MKUBWA DUNIANI KAMA KUWA NA MTOTO: Ona nilivyovaa - TopicsExpress



          

HAKUNA UTAJIRI MKUBWA DUNIANI KAMA KUWA NA MTOTO: Ona nilivyovaa suti nzuri ni matunda ya kuwa na mtoto. Nikiumwa mara moja napokea pesa kwa m-pesa naujumbe ya kwamba baba nenda hospitali. Nakuhakikishia kijana wangu kuna mambo ambayo watoto wangu wamenisaidia ndiyo maana nadhubutu kukuambia kuwa watoto ni utajiri mkubwa. Kwa mfanoleo hii nikienda Arusha watoto wangu, watu niliowajengea nyumba wananipokea kama rais obama. Kwangu mimi huu ni utajiri mkubwa kijana wangu. Nisamehe kama nimekukwaza Kimambo lakini nakuomba unielewe kuwa mtoo ndio utajiri mkubwa kuliko yote duniani hata kama una ndoto za kuwa padri nisamehe ila nakuhusia mtoto ndio utakuwa utajiri wako mkubwa hapa duniani. Mzee,injinia Mkonyi ni mzee mwenye umriwa miaka 78na anaishi Moshi mkoani Kilimanjaro. Ni moja ya wazee wanaoheshimika sana hapa tanzania na hata baadhi ya nchi za africa mashariki kwani akiwa na umri wa miaka 26 aliweza kukaa nchini kenya akijishughulisha na ujenzi wa maghorofa mbalimbali katika miji ya Eldoreti.
Posted on: Sat, 24 Aug 2013 16:53:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015