HATIMAE MWALIMU ANAELEKEA UKOMBOZI, JE FEDHA ZILIZOKATWA KINYUME - TopicsExpress



          

HATIMAE MWALIMU ANAELEKEA UKOMBOZI, JE FEDHA ZILIZOKATWA KINYUME CHA SHERIA TUMWACHIE NANI? TTN INAANDAA MKAKATI WA MADAI YA FEDHA ZOTE ZILIZOKATWA KINYUME CHA SHERIA NA MADAI YA RIBA YA FEDHA HIZO...JE NANI AWAJIBIKE? SERIKALI AU CWT? HII ITAKUWA KESI KAMA YA MAUMAU! NEWS; WARAKA KUTOTOKA OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAH: WARAKA WA UTUMISHI WA UMMA NA.1 WA MWAKA 2013 KUHUSU MAKATO YA ADA ZA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUTOKA KATIKA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI UTANGULIZI 1.Kwa mujibu wa kifungu cha 9 cha sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6/2004 Wafanyakazi wanayo haki ya kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi au kuanzisha Chama cha wafanyakazi kwa kuzingatia matakwa ya yaliyowekwa katika Kifungu cha 46 na 47 cha sheria hii. 2.Utaratibu wa makato ya ada za Vyamavya wafanyakazi kutoka katika mishahara ya watumishi umeelekeza katika kifungu cha 61(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6/2004 . Kwa mujibu wa Kifungu hicho , Mwajiri atapaswa kukata ada ya Chama cha Wafanyakazi kilichosajiliwa kutoka kwenye mshahara wa Mwajiriwa kama mwajiriwa amemwadhinishia mwajiri afanye hivyo katika fomu iliyoelekezwa ambayo ni TUF6. fomu hii inapatikana kwenye kanuni za Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini mwaka 2007. 3. Kwa mujibu wa Kifungu cha 61 (4) cha Sheria hiyo, mwajiriawa anaweza kubatilisha idhini ya makato ya mshahara wake kwa kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa mwajiri na Chama cha Wafanyakazi . Aidha endapo mwajisriwa amebatilisha idhini hiyo chini ya Kifungu cha 61(4) Kifungu cha 61(5) kinamwelekeza mwajiri kuacha kukata makato yoyote baada ya muda wa taarifa kuisha yaani mwezi mmoja. 4. Kila mwezi wa kuwasilisha makato hayo, mwajiri atakipatia Chama cha Wafanyakazi. (i) Orodha ya majina ya wanchama katika fomu iliyoeledezwa ya wale ambao kakato yao yanatakiwa kufanyika na (ii) Nakala ya taarifa yoyote ya kusitisha makato chini ya kifungu cha 61(4) MADHUMUNI YA WARAKA HUU 8. Madhumuni ya Waraka huu ni kuwakumbusha Waajiri wote ambao wana jukumu kisheria la kukata ada kutoka katika miashara ya Wafanyakazi walio chini yao, utaratibu wa kushughulikia makato ya ada ya Vyama vya Wafanyakazi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zinazotawala Ajira na Mahusiano Kazini. 9. Ili kusimamia utaratibu wa utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6/2004 ipasavyo, Waajiri watapaswa kuuzingatia yafuatayo : (i) Kuwaelimisha wafanyakazi hususan waajiriwa wapya juu ya umuhimu wa vyama hivi, (ii) Baada ya kupata maelezo na mtumishi kuidhinisha kukatwa mshahara wake, mtumishi atajaza na kusaini Fomu Maalumu(TUF 6) ya kuidhinisha makato kutoka katika mshahara wake . Waajiri hawatapaswa kukata mishahara ya watumishi kabla ya mtumishi hajajaza na kuweka saini yake katika Fomu Maalum ya TUF 6, (iii) Kuhakikisha kuwa makato ya Watumishi waliobatilisha kukatwa ishahara yao na ambao wmetoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja hawakatwi mishahara yao, Kuwasilisha Fomu na majina ya watumishi waliokatwa ada kwa mwezi katika Chama cha wafanyakazi alichochagua mfanyakazi kujiunga nacho na kubakia na nakala katika Ofisi ya Mwajiri, na (iv) Waajiri wanapaswa kuhakikisha kuwa wanawasilisha makato hayo kwa Vyama vya Waafanyakazi bila kukosa. MENGINEYO 10. Waajiri wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa kusimamia ipasavyo utaratibu wa makato ya ada za Vyama vya Wafanyakazi kutoka katika mishahara ya Wafanyakazi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6/2004. ili kuepusha migogoro kazini . Mwajiri atakayekiuka utaratibu huu, atakuwa anavunja Sheria na hivyo Serikali itawachukulia hatua stahiki. 11. Kwa kuwa Serikali imeanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za Rasilimali watu na Malipo ya Mishahara, Waajiri wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa fomu iliyotajwa katika aya ya 2 ya Waraka uu tarhe 1 Julai, 2013 kwa kuwa baada ya tarehe hii, Mfumo hautamkata mfanyakazi yeyote abaye hajaidhinisha kukatwa mshahara wake. UTEKELEZAJI 12. Waraka huu utasomwa kwa pamoja na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6/2004 na Kanuni zake za mwaka 2007 na utaanza kutumika rasmi tarehe 1 Julai, 2013.
Posted on: Sat, 29 Jun 2013 07:36:43 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015