Hivi majuzi Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amewaahidi wakazi - TopicsExpress



          

Hivi majuzi Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko amewaahidi wakazi wa mtaa wa Korogocho kuwa yeyote atakayesalimisha bunduki kwake atakabidhiwa shilingi elfu 50 (sh50,000). Na leo mkazi mmoja amempa Sonko bunduki aina ya AK 47. Kwa kuwa ahadi ni deni na dawa ya deni ni kulipa, Sonko amempa pesa taslimu za Kenya, shilingi elfu 50! Je, njia hii mpya itapunguza visa vya uhalifu jijini Nairobi? Jiunge na Sonko mwenyewe na mwanahabari Ahmed Dharwesh katika #KTNLEO saa moja kwa mjadala wa kina kuhusu suala hili.
Posted on: Fri, 20 Sep 2013 15:21:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015