Hongera Maswi,Mzee Mengi kuwa wazalendo kutetea uzawa katika - TopicsExpress



          

Hongera Maswi,Mzee Mengi kuwa wazalendo kutetea uzawa katika ugawaji wa vitaru vya gesi......kauli ya waziri Muhongo kwamba watanzania ni wafanyabiashara wa juisi na maji hawana uwezo kuwekeza kwenye gesi si kauli ya kizalendo.....mimi ni kati ya watanzania ninayeamini kwamba nchi siyo jina wala bendera wala jeshi bali nchi ni uzawa...nchi,uhuru,maendeleo maana yake ni wazawa kumiliki rasilimali zao.nawapongenza sana mzee mengi na mh.Maswi kusimamia sheria ya kuwawezesha wazawa kupewa kipaumbele katika ugawaji wa vitalu vya gesi.Nataka nipingane na mh Muhongo kwamba uwekezaji ni mtaji wa pesa tu,uwekezaji wa dunia ya leo si mtaji wa pesa au wazungu,wachina .....wageni bali ardhi ,elimu ni mtaji tosha.Hata Baba wa Taifa aliwai kusema madini yapo ila wazawa wapate elimu kwanza ili waje kumiliki rasilimali zao.Dubai ilivyojengeka yale magorofa yote si waarabu bali wazawa wameingia ubia na wageni hata Libya mafuta yao waliweka uzawa mbele.Ninayo imani kitalu pekee(ardhi) ni zaidi ya 50 percent ya mtaji.watanzania tubadilike kifikira tuamini kwamba tunaweza tusitegemee wageni ndo watujengee nchi yetu,rasilimali zetu zinatosha kujenga nchini kama tutaamini kwenye uzalendo.
Posted on: Sat, 21 Sep 2013 09:30:39 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015