Ilipoishia Yule mama aliniambia "pumzika kwanza alafu badae ndo - TopicsExpress



          

Ilipoishia Yule mama aliniambia "pumzika kwanza alafu badae ndo utaonyeshwa mazingira ya kazi alafu wekeend nikumbushe nikakufanyie shoping sijapenda hizo nguo ulizovaa" Endelea SEHEMU YA PILI Nilifurahi sana kusikia vile sababu ni kweli nguo nilizokuwa nimevaa zilikuwa zimechakaa zimepauka zina viraka hadi nilikuwa naona aibu kukaa pale kwenye lile sofa nilihisi kama nachafua Yule mama akaniambia "hapa ndani kuna house girl ndo huyo aliekuja kuwapokea pale getini huyo mzee unayemuona hapo ndo mume wangu pia kuna mabinti zangu wawili wanasoma bording ila kila weekend wanarudigi hapa nyumbani kwa hiyo wote hao waheshimu wachukulie kama ndugu zako ishi nao vizuri" nikamwambia "sawa mama ninekusikia" alimuita yule housegirl akamuambia akanionyeshe chumba changu ambacho nitakuwa nalala kilikuwa nje kabisa lkn nilikipenda sana kilikuwa ni chumba kikubwa kisafi kilikuwa na vitu ambavyo nilitamani na mm siku moja niwe navyo kilikuwa na Tv,Radio na kitanda kikubwa kilichotandikwa mashuka mazuri kwa kweli nilikifurahia sana kile chumba japo vitu havikuwa vyangu siku ile sikufanya kazi yyte nilikuwa naelekezwa tu kazi ambazo nitakuwa nazifanya yule mama alikuwa na mifugo ya aina mbalimbali akaniambia kazi yangu kubwa itakuwa ni kuiangalia ile mifugo na kuhakikisha ipo salama Ulifika usiku tukala chakula cha pamoja chakula ambacho nilikuwa nakionaga tu watu wanakula na sikutegemea kama siku moja na mm nitakula msosi wa maana vile siku ile house girl alituandalia kuku rost wali maini mboga za majani zilizopikwa vizuri na juice nzuri ya maembe pamoja na matunda ya aina mbalimbali nilikula hadi nilijisikia raha Kidogo kidogo nikaanza kuyazoea mazingira ya ile nyumba nikaacha kushangaa shangaa kila nilichokiona niliona kawaida tu Ilifika siku ambayo nilikuwa naingojea kwa hamu siku ya mm kufanyiwa shoping Ilikuwa ijumaa mchana yule mama akaniambia "cox jiandae twende tukawachukue wanangu shule tupitie na kariakoo ukafanye shoping" nilimalizia kazi zangu haraka nikajiandaa yule mama na yeye akajiandaa akaniuliza "hivi cox unajua kuendesha gari?? Nikamwambia "hamna mama hata sijui" akaniambia "nilijua unajua nilitaka uniendeshe lakini usijali tutatafuta mtu akufundishe"nilifurahi sana kusikia vile sababu nilitamani sana siku na mimi nijue kuendesha gari Tulipanda gari ya yule mama hadi shuleni wanaposoma mabinti zake tuliwakuta wapo getini wanatusubiri tukapakia mabegi yao ndani ya gari na wenyewe wakapanda tukaanza safari wale mabinti wa yule mama walikuwa wananiangalia sana hadi nikaanza kujistukia nikajua wananishangaa manguo yangu mabaya niliyoyavaa mmoja akamuuliza mama yake "mama huyu ni nani mbna sisi hatumjui?? Mama yao akawaambia"huyu ni house boy pale nyumbani anaitwa cox muheshimuni kama kaka yenu" Inaendelea GONGA LIKE KAMA UMEIPENDA STORY UNATAKA IENDELEE
Posted on: Sun, 29 Sep 2013 14:02:02 +0000

Trending Topics



style="min-height:30px;">
Indian Group Calls Kashmir ‘Disputed Region’, Calls
Delirante articolo di Scalfari contro il M5S: Se vince Grillo,
على ما الليل ليل , كانو الشهدا 24
AMIGOS DEL JUDO, MUCHOS MENSAJES ESTAN LLEGANDO Y TODOS ME
Dragi susținători ai cauzei noastre, Odată cu noua
mezelet a3bed tetsawer b lunette fi dar ? mezelet bnet tekteb esm
We just learned today that my new Pom Q has his first litter on

Recently Viewed Topics




© 2015