JOYCE KIRIA AELEZEA SAFARI YAKE YA TABORA KUMWONA MUME WAKE - TopicsExpress



          

JOYCE KIRIA AELEZEA SAFARI YAKE YA TABORA KUMWONA MUME WAKE ILIVYOKUWA Safari yangu kuelekea mkoani tabora ilikuwa na changamoto nyingi, Ila kubwa namshukuru Mungu nilifika salama na kurudi salama. Najua kuna FANS wangu wengi wananipa support haswa katika maombi ya familia yangu. So najua itakuwa vizuri kama nitashare na nyie jinsi safari yangu nzima ilivyokuwa. Nimetumia siku tano so nitakuwa naielezea kwa day after day ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka naenda mpaka narudi. Si mabali kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5 hivi kwa Gari, tukawa tumefika gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata kujiandikisha na kila kitu halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana pia tulikuta watu wengine ambao nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na sie tukaitwa katika listi tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria zao za kuzima simu na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko kijichumba kidogo tu. Kiukweli it was a very SAD moment, nilipomuona mume wangu, akiwa kwa upande wa pili na sikuwa namuona vizuri mana hiyo nyavu iliyotenganisha hapo ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa Kujizui MACHOZI yalianza kunitoka, Ila mume wangu alikuwa MORE THAN STRONG akinisihi nisilie ye yuko poa, Kiukweli Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na mie Napata nguvu. Swali la Kwanza aliniuliza Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako salama , Kutokana na umbali wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia Naendelea Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko Upande Wetu, Misukosuko niliyoipata njiani nawaza ningekuwa na watoto ingekuwaje”?? .Tukaongea mawili matatu kama dakika tano hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka. Kuna nguo nilibeba tukaambiwa zikakaguliwe kwanza then ndo atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka then tukaondoka. Kiukweli after kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia kuwa yuko mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache sana na nilikuwa na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale wakatuambia kwa waliotoka mbali huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at least hata dk kumi, so nikipanga kurudi tena siku ya Jumatatu.
Posted on: Sat, 06 Jul 2013 09:52:17 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015