Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) - TopicsExpress



          

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wanafanya kikao maalum cha dharura cha Baraza kuu la Taifa katika afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar. Kikao hiko maalum kinalenga kujadili baadhi ya hoja za msingi kwa mustakabal na uhai wa jumuiya hiyo, ajenda hizo ni pamoja na kupitisha jina la Katibu Mkuu mteule wa jumuiya hiyo Ndugu Sixtus Mapunda. Viongozi mbalimbali wa Chama na Jumuiya zake zikiwemo za wazazi na wanawake, viongozi wastaafu wa jumuiya ya vijana na viongozi wapya wateule wa jumuiya za Chama wamehudhuria kikao hicho maalum cha baraza kuu la UVCCM Taifa. Viongozi hao ni Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Iddy, Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahaman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM zanzibar Ndugu Alli Vuai, Katibu wa Oganaizesheni wa CCM Taifa Ndugu Seif Khatibu, Waziri wa nchi ulinzi na usalama ndugu Emmanuel Nchimbi, waziri wa sayansi na teknolojia Ndugu January Makamba, waziri asiye na wizara maalum znz ndugu Machano Othman Said na katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi na naibu katibu mkuu wa jumuiya hiyo. Kikao hiko kinaendelea hivi sasa ambapo viongozi mbalimbali wanatoa nasaha zao na kisha ajenda za kikao hiko kuanza kujadiliwa. Sambamba na Kikao hicho maalum Cha Baraza pia kutakuwa na mkutano wa hadhara ambao utahutubiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge Ndugu Sadiffah Juma Khamis katika uwanja wa Kombawapya uliopo wilaya ya mjini Zanzibar.
Posted on: Sun, 01 Sep 2013 10:06:44 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015