KATIKA ITV JUMATANO TAREHE 3/07/2013 1:00 USIKU Fuatilia - TopicsExpress



          

KATIKA ITV JUMATANO TAREHE 3/07/2013 1:00 USIKU Fuatilia kipindi maalum cha wizara ya nishati na madini kikiongelea umuhimu wa nishati za mafuta na gesi kwa taifa. Kama kweli tunataka kuondokana na umasikini, ni lazima kuwekeza kwenye nishati hizo. Ndio mkombozi wetu. 3:10 USIKU Usipitwe na kipindi maalum cha Uongozi na ufuatilie mazungumzo bayana na Dk Gro Brundtlan waziri mkuu wa zamani wa Norway akizungumzia changamoto alizokutana nazo akiwa mwanamke wa kwanza kuwa na cheo cha waziri mkuu nchini humo. 4:00 USIKU Katika muendelezo wa tamthilia ya kusisimua ya RUBI, akiwa hana ili wala lile, Maribel amfuma Rubi akiwa kava gauni lake aliloandaa kwa ajili ya kuvaa siku ya harusi yake na Hector. Mshituko mkubwa wampata. Na penzi la siri la Rubi la Hector lazidi shika kasi. Fuatilia 5:30 USIKU Usikose kuangalia muendelezo wa tamthilia ya kusisimua ya 24, Karen mke wa Bill mkuu wa CTU amueleza mumewe kajiuzulu. Je, Bill atajua sababu ya maamuzi hayo ya mkewe?. Na je atakubaliana nayo? Na jack Bauer aweka undugu pembeni na kumshikisha adabu kaka yake akitafuta ukweli wa kuhusika kwake na suala zima la ugaidi. KWA VIPINDI SAFI,VINAVYOSISIMUA, KUELIMISHA NA KUBURUDISHA, ANGALIA ITV PEKEE. UNAWEZA KUTUFUATILIA KUPITIA itv.co.tz. KWA MAONI NA USHAURI TUANDIKIE [email protected]
Posted on: Wed, 03 Jul 2013 07:30:05 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015