KIEMBA ::: MMECHEMKA KUMUACHA KASEJA KIUNGO wa Simba ambaye - TopicsExpress



          

KIEMBA ::: MMECHEMKA KUMUACHA KASEJA KIUNGO wa Simba ambaye anatakiwa na klabu ya Raja Casablanca ya Morocco, Amri Kiemba amewaambia viongozi wa klabu hiyo kwamba hajafurahishwa kuachwa kwa kipa namba moja, Juma Kaseja. Kiemba ambaye amesaini mkataba na Simba kwa Sh.35 milioni, amesisitiza kuwa uamuzi uliofanywa dhidi ya Kaseja kwa mtazamo wake si sahihi labda kama kuna sababu nyingine ya nje ya uwanja. “Sijafurahishwa na uamuzi waliofanya viongozi wa kumuacha Kaseja, kusema kweli si sahihi kwa sababu Kaseja bado naamini ni kipa mzuri na ana uwezo mkubwa sana na isitoshe hakuna sababu ya maana iliyowafanya wamuache labda kama kuna sababu nyingine pembeni na si ya kisoka,” alisema Kiemba ambaye aliwahi kucheza Yanga. Aliongeza: “Hili jambo nimelisikia tu juu juu ingawa sasa naanza kuamini ingawa viongozi kokote walipo wajue hawajatenda haki bado alistahili kuichezea timu hii.” Kaseja alianza kuichezea Simba mwaka 2003 akitokea Moro United na aling’ara mwaka huo wakati wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kuiingiza klabu hiyo kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuitoa Zamalek ya Misri kwa penalti. Simba wamethibitisha kupitia kwa Mwenyekiti wa klabu, Ismail Aden Rage na bosi wa usajili, Zakaria Hanspope kwamba hawatampa Kaseja mkataba mpya na kwamba akatafute timu nyingine.
Posted on: Sat, 29 Jun 2013 06:16:04 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015