Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran, Ayatullah - TopicsExpress



          

Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa mjini Tehran, Ayatullah Muhammad Imami Kashani, amesema kuwa, ili kuzuia mauaji zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu ni wajibu wa maulama na wasomi wa Kiislamu, kukabiliana na fikra za kueneza ukatili zinazoenezwa na Mawahabi wa Kisalafi wanaowakufurisha Waislamu wenzao duniani. Sambamba na kuonya juu ya ongezeko la fikra za kukufurishana za Uwahabi katika Uislamu, Ayatullah Imami Kashani amesema kuwa, maulama na wasomi wa Kiislamu wanatakiwa kukabiliana na tishio hilo, kwa kutumia hatua za lazima zikiwemo pia za kielimu. Ametahadharisha juu ya hali ya kusikitisha mno katika nchi za Kiislamu hususan Misri na Syria na kusema, matukio ya hivi karibuni yanaonyesha wazi kuwa, ulimwengu wa Kiislamu una maadui wengi. Khatibu wa Sala ya Ijumaa Ayatullah Muhammad Imami Kashani, amesema kuwa, mauaji ya na ukatili wa Masalafi wa Kiwahabi, vilianza tangu mwanzoni mwa karne ya tatu huku Uingereza katika fremu ya kupanua siasa zake za kupenda kujitanua, ikifanya njama kubwa katika kulea na kupanua fikra za kundi hilo katika ulimwengu wa Kiislamu. Ameashiria pia juu ya hali ya mambo huko nchini Misri kufuatia kuuzuliwa Muhammad Mursi, rais wa zamani wa nchi hiyo na kusema, hii leo walimwengu wanashuhudia namna gani firauni anavyokuja na kulifanyia khiyana taifa na kisha pamoja na yote hayo anaachiliwa huru.
Posted on: Sat, 24 Aug 2013 07:23:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015