Kijamiii #1-Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekutana na viongozi wa - TopicsExpress



          

Kijamiii #1-Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amekutana na viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Kenya (SUPKEM) na kuwahakikishia kuwa serikali yake itatoa huduma bora kwa Wakenya wote. Katika mkutano huo uliofanyika Ikulu ya Rais mjini Nairobi jana Jumatano, Rais Kenyatta alisema hakuna Mkenya atakayebaguliwa kwa msingi wa dini, kabila au msimamo wa kisiasa. Amewahakikishia Waislamu kuwa hawatatengwa au kubaguliwa na hivyo amewataka kuimarisha nafasi yao katika ujenzi wa taifa. Viongozi wa Supkem wakiongozwa na mwenyekiti wao Profesa Abdulghafur el Busaidi walimfahamisha Rais Kenyatta kuhusu masuala ambayo Waislamu wanataka serikali iyashughulikie. Kati ya viongozi waandamizi wa SUPKEM waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Supkem Adan Wachu na Makamu Mwenyekiti kitaifa Alhaji Abdullah Kiptanui. Mkutano huo ulikuwa wa kufuatilia majadiliano yaliyofanyika katika mwaliko wa dhifa ya futari iliyofanyika katika Ikulu ya Rais mjini Nairobi Jumamosi iliyopita. ======. #2-Mahakama ya Kimataifa ya Jinai za Rwanda ICTR imeikabidhi Rwanda mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki katika fremu ya uamuzi wa mahakama hiyo kuhamisha kesi za mahakama hiyo. Msemaji wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Rwanda Alain Mukurarunda amethibitisha kuwa mtuhumiwa Bernard Munyagishari aliwasili Kigali Jumatano. Munyagishari alikuwa Katibu Mkuu wa chama tawala cha zamani MRND katika eneo la Gisenyi wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Aidha alikuwa mkuu wa tawi la vijana la chama hicho yaani Interahamwe. ICTR inasema Munyagishari alihusika na kupanga njama ya mauaji ya umati, ubakaji na jinai dhidi ya binaadamu. Mwaka jana ICTR iliikabidhi Rwanda mtuhumiwa mwingine wa mauaji ya kimbari ambaye ni Jean Uwinkindi, Kasisi wa Kanisa la Kilokole. ICTR yenye makao yake Arusha Tanzania inatekeleza sera ya kuzikabidhi mahakama za Rwanda jukumu la kusikiliza kesi za washukiwa wa mauaji ya kimbari. Mahakama hiyo inapaswa kumaliza kazi zake ifikapo mwisho wa mwaka 2014. Awali ICTR ilikuwa na wasi wasi kuhusu iwapo watuhumiwa hao watapata uadilifu katika mahakama za Rwanda lakini mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ilibadilisha mtazamo wake kufuatia marekebisho katika vyombo vya mahakama vya Rwanda. #3-Idadi ya waliouawa katika ajali ya treni nchini Uhispania imeongezeka na kufika watu 77 huku mamia ya wengine wakijeruhiwa baada ya treni hiyo ya abiria kuacha reli. Ajali hiyo imetokea katika mji wa Santiago de Compostela katika mkoa wa Galicia. Mabehewa 13 ya treni hiyo yaliondoka katika reli na manne yamepinduka kabisa. Treni hiyo iliyokuwa na abiria 218 ilikuwa ikitoka Madrid kuelekea El Ferrol na hali ya baadhi ya majeruhi inaripotiwa kuwa ni mbaya sana. Ajali hiyo imetajwa kuwa mbaya zaidi ya treli nchini Uhispania katika kipindi cha miaka 40 iliyopita. Serikali ya Uhispania inachunguza sababu ya ajali hiyo. Ripoti za awali zinasema treni hiyo iliacha reli kutokana na mwendo wa kasi. #3- Tarehe 20 Julai, 2013 kulitokea mauaji ya mfanyakazi wa mgodiwa Tanzanite ulioko kitalu C, Mirerani wilayani Simanjiro kwakupigwa risasi na mchimbaji kutoka mgodi wa wachimbaji wadogowa kitalu D katika eneo hilo.Kitendo hicho kimetokana na wachimbaji wadogo wanaopakanana Kitalu C kuvuka mipaka ya vitalu vyao na kuendesha uchimbajindani ya Kitalu C, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Madiniya Mwaka 2010 na Kanuni zake.Kwa sasa Kitalu C kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Madinila Taifa (STAMICO) na Kampuni ya Tanzanite One kwa asilimia 50kwa 50. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hatua za kisheriazitachukuliwa kwa wale watakaobainika kuhusika. Wizaraimesikitishwa sana na mauaji hayo ambayo ni ukiukwaji wataratibu za usalama migodini.Serikali haitavumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea nakuhatarisha usalama wa wachimbaji katika migodi ya TanzaniteMirerani. Tunapenda kuwatangazia wamiliki wa migodi yote ya wachimbajiwadogo katika vitalu B na D ambayo uchimbaji wake unafanyikandani ya mipaka ya Kitalu C kuwa wasitishe shughuli zao maramoja na wahakikishe kuwa uchimbaji unafanyika ndani yamipaka ya vitalu vyao.Aidha, uchimbaji uzingatie taratibu za usalama migodini ikiwa nipamoja na kutojihusisha na utumiaji wa silaha za aina yoyotemigodini. Ukaguzi wa migodi kubaini migodi inayoendeshauchimbaji ndani ya mipaka ya kitalu C utafanywa na Timu yawataalam wa Wizara ya Nishati na Madini. Vitalu vitakavyobainikakuhusika leseni zake zitafutwa na uchimbaji utatakiwa kusitishwakatika migodi hiyo
Posted on: Thu, 25 Jul 2013 17:54:48 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015