Kuna wapenzi waliopendana sana na wakaamua kuoana lakini Kijana ni - TopicsExpress



          

Kuna wapenzi waliopendana sana na wakaamua kuoana lakini Kijana ni Mkristo na msichana ni Muislamu.Walipata mtoto kabla ya kuoana na walipoenda kwa babake msichana ili waweze kuoana,Mzee akakataa mwanawe aolewe na Mkristo,msichana alisisitiza kwamba hatokubali kuolewa na mtu mwengine kama si huyu Mkristo na mwishowe akafukuzwa na babake.Msichana alienda kwa yule mpenzi wake na wakaishi pamoja na mtoto wao na baada ya mwezi kupita babake msichana aliwaita wote wawili na walipofika akamwambia Yule kijana kwamba itabidi amsilimishe ndio amruhusu kumuoa mwanawe naye Kijana akasema hatobadili dini kwani wenyewe walikua wamependana bila kigezo cha dini.Baba ya msichana alimuzuia mwanawe pale nyumbani na kumwambia kijana iwapo hataki kusilimishwa basi atamtaftia bintie mume muislamu.Sasa mume ashapatikana na msichana hataki anamtaka yule Mkristo.Ndio wanataka ushauri wafanyeje wapenzi hawa?Voroni ukiwa na Dama na Kalambua?
Posted on: Fri, 13 Sep 2013 03:12:16 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015