MIFUMO MIBOVU YA SERIKALI IMECHANGIA KUZOROTESHA SANAA. Jamii - TopicsExpress



          

MIFUMO MIBOVU YA SERIKALI IMECHANGIA KUZOROTESHA SANAA. Jamii Wilayani Kilombero imeshauriwa kuwekeza katika sanaa na kutambua kuwa sanaa ni ajira. Ushauri huo umetolewa na Mwanzilishi wa kituo cha nyumba ya sanaa Ifakara Bwana Said Mwendabwila alipokuwa akizungumza na pambazukofm. Mwendabwila amesema kuwa jamii haitambui kuwa sanaa ni ajira na hiyo imetokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya mambo mbalimbali yanayohusu sanaa. Aidha amesema Wasanii wengi wa Tanzania wameshindwa kufikia malengo kutokana na serikali kushindwa kuiendeleza sanaa ambapo sababu kubwa imetokana na mifumo mibovu. Akitolea mfano wa kimfumo, amesema miaka ya hivi karibuni serikali iliondoa mashindano ya michezo mashuleni hali hiyo imechangia kuuwa vipaji kwa vijana waliokuwa na moyo wa kuviendeleza vipaji vyao. Amesema sababu nyingine ya kushuka kwa sanaa hususan uchoraji ni kutokuwepo kwa vituo vya sanaa ambavyo vitawafanya vijana wengi kujiunga na kujifunza sanaa hiyo. Kwa mujibu wa mwendabwile amesema kwa mkoa mzima wa morogoro una kituo kimoja cha sanaa ambacho kipo ifakara kinajulikana kwa jina la ELITAYE DIPILO CULTURE ikiwa ni kumbukumbu ya mwalimu aliyekufa kwenye maonyesho ya sanaa Nchini Italy akionyesha kazi za msanii wa Ifakara,na hiyo ndiyo iliyopelekea fedha yake kujenga kituo hicho.
Posted on: Thu, 14 Nov 2013 08:25:12 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015