MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI SEHEMU YA - TopicsExpress



          

MWANAMKE MWENYE KOVU JEUSI SEHEMU YA 21 ************************ ********** Nilifika kwangu usiku ule mida ya saa mbili usiku baada ya kuoga nilivaa nguo mahususi kwa ajili ya kulalia kisha nikwa nimekaa naangalia taarifa ya habari, mara simu yangu ikaita alikuwa ni Amina akinijulisha ya kwamba alikua anaomba kama inawezekana nimsaidie kumpeleka kwake sinza mori kwani alikuwa na vitu vingi halafu alikuwa amekaa zaidi ya saa toka nilipomuacha pale stendeni ya vidaladala stesheni bila ya gari yoyote kuja, niliona si mbaya kwani Amina alikuwa ni mmoja ya wadada niliokuwa nao karibu sana pale kazini yeye pamoja na Jamila ambaye Jamila ni mdada niliyekuwa nampenda sana toka nilipomjua kwani alikuwa ni mkimya sana huku akiwa ni mtu asiyekuwa na makuu sema kwa kipindi kila Jamila alikuwa ameenda nchini marekani kwenye course ya social intelligence kwa takiribani miezi mitatu, muda mwingine nilikuwa namkumbuka sana Jamila kwani achilia mbali na kumpenda ila alikuwa ni mchapakazi na huku akili yake ikiwa nyepesi sana katika kuchambua mambo. Nilimkuta pale stesheni Amina na kumchukua na gari yangu ili kumuwahisha kwakeambapo alikuwa akiishi peke yake kwa maana nay eye pia aliniambia atajitahidi kesho kuwahi hata kwa kutumia taxi wani alikuwa hajafanikiwa kununua gari, ili tuje tusaidiane katika lile paredi la utambuzi, basi tulienda taratibu kutakana na foleni huku tukipiga story mbali mbali tulifika kwake ilikuwa ni mida ya saa 4 hivi usiku basi wakati tumepaki gari nje tuliona taa za ndani kwake zikiwa zimeweka,Amina alishituka na kuniambia ya kwamba yeye pindi alipoondoka alicha taa amezizima, wakati tunajishauri mara kwa ndani kupitia dirishani tuliweza kumuona mtu kwa mbali ambaye baada ya kuona gari imesimama nay eye alichokifanya ni kuzima taa mule ndani hivyo basi tukakosa ujanja wa kuingia ndani kwa maana tusingeweza kuingia ndani wakati mtu Yule amezima taa na hatukujua ni nani na alikuwa na silaha gani. Tulishauriana pale huku tukiwa hatuna la kufanya hatukutaka kuita watu kwanza tulijua tu atakuwa ni mwanamke mwenye kovu jeusi atakuwa ameingia kutegesha vinasa sauti vyake au kufanya upekuzi kama ilivyokuwa ada yake. Lakini kitu kilichotushangaza ni jinsi alivyoweza kucheza na muda kwani mara zote kila alipoenda sisi hatukuwepo sasa tulijiuliza kwa siku ile alijuje kama Amina atachelewa kazini. Tulijadiliana pale kwa zaidi ya saa zima kwani yle mtu alikuwa kama akitufanya watoto akiwasha simu na kuzima mara ya chumbani mara ya jikoni mara ya sebuleni ili mradi tu kutuchanganya kisha nikamwambia Amina liwalo na liwe nikamuomba bastola yake kisha nikachungua fungua na kuanza kuingia mule ndani, nilifungua mlango na kuwasha taa pale sebuleni sikuweza kumuona mtu, palikuwa pametulia tulii, nilijaribu kutazama tena kwenye korido sikuweza kumuona mtu, nilielekea jikoni wakati natokea tu nikaona mlango wa kule jikoni uliokuwa ukitoka nje pia ukifunguliwa na mtu akitoka kwa kasi ya ajabu akikimbia kulekea barabarani basin a mimi sikutaka kupoteza muda nilitoka nje ambapo aliniona nikija kwa kasi kumbe alikuwa makuja na piki piki akawa ameipaki nyuma ya ile nyumba aliponiona nakuija kwa kasi alishindwa hata kuipanda ile pikipiki na kuanza kukimbia kwa miguu akielekea barabarani, sikutaka kumuacha nilianza na mimi kumkimbiza huku nikimjulisha Amina kwa sauti sina hakuka kama alinisikia nilimkimbiza alishika barabara akawa kama anaelekea sinza parestina alikuwa na mbio za ajabu zijawahi kuona, nilizidi kumfuata kwa kasi ya ajabu huku bastola ikiwa tayari tayari mkononi na kwa muda mule barabara ilikuwa imeshakuwa nyeupe kwani watu wengi walikuwa maeshalala ilikuwasaa sita hivi inaelekea saa saba usiku, basi Yule mtu alipofika sinza makaburini alisimama kidogo na kuningalia kama nilikuwa bado namfuata aliponiona nilikuwa bado namfuata akakimbilia ndani ya makaburi, namimi sikutaka kujifikiria nilipofika pale na mimi nikaingia mule makaburini, sikuweza kumuona tena mule kila upande nilipoangalia hakuonekana, basi nikasimama mule makaburini kwa muda wa kama sekunde tano huku mapigo ya moyo yakianza kuongezeka nikasogea mbele kama hatua nane hivi palikuwa na kaburi kubwa ambalo lilikuwa limejengwa kifahari sana na likiwa limeinuka juu ambalo lilikuwa chini ya mti mkubwa wa mkuyu, nilimuangalia kama alikwa labda amejificha pale mbele ya lile kaburi lakini sikumuona, nilijikuta nakata tamaa na kuona potelea mbali haikuwa siku yake kumkamata basi nikageuka ili niludi kwa Amina niende zangu nikalale,mungu wangu kila nilipojaribu kupiga hatua nilihisi kama kuna kitu kinanivuta kwa nyuma,nilisimama nikajua kama ni Yule mtu basi atazungumza kitu au atafanya jambo lolote,nilisubili kwa muda wa zaidi ya dakika 5 bila kusikia wala kuhisi lolote nikajaribu kupiga hatua tena niondoke lakini wapi nilijikuta navutwa tena. Mwili ulianza kusisimka kwa maana sehemu yenyewe niliyokuwa ni makaburini palikuwa panatisha na ni usiku nilianza kujisemesha pale ili kama ni Yule mtu basi anijibu lakini wapi palikuwa kimya sana,huku upepo tu ukivuma kwa mbali,nilijaribu tena kupiga hatua kusogea mbele lakini wapi bado nilivutwa hapo hapo nikajua mwisho wangu umefika tayari…..!! ITAENDELEA KESHO SAA 4
Posted on: Thu, 18 Jul 2013 18:27:57 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015