Mama: Mwanangu hebu mpigie simu baba yako mwambie chakula - TopicsExpress



          

Mama: Mwanangu hebu mpigie simu baba yako mwambie chakula tayari. Mtoto: Sawa mama. Basi mtoto akampigia simu baba yake lakini hakumpata. Mtoto: Mama simpati. Mama: Basi subiri kama baada ya dakika tano mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.Baada ya dakika tano mtoto akampigia tena baba yake. Mtoto: Mama mimi baba simpati simu yenyewe anapokea mwanamke. Mama: Heeh! sawa mwanangu niachie mimi hili suala wewe nenda kale. Baada kama ya dakika 30 baba akabisha hodi akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizuri akapigwa na sufuria mara mwiko ikawa ni balaa kwa kwenda mbele mume akazidiwa mara majirani wakaja kuamulia ugomvi, lakini majirani walipofika wakakamkuta mume yuko chini ya sofa hoi bin taaban. Mama: Pumbavu zako we wa kunifanyia mimi hiviyaani unakwenda kwa malaya zako na kuniacha mimi hapa nyumbani? Mwanangu hebu waambie majirani yule mwanamke alipo pokea simu alisemaje? Mtoto: Alisema simu uliyopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena baadae! Unadhani kilifuata nini?? Usisahau kulike na ku share..
Posted on: Tue, 16 Jul 2013 04:16:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015