Mbeya City... Mbeya City... Mbeya City!! Najaribu kuifikiria kasi - TopicsExpress



          

Mbeya City... Mbeya City... Mbeya City!! Najaribu kuifikiria kasi ya #Mbeya_City, kama kawaida yangu mimi ni mnazi sana wa gazeti la Mwanaspoti,leo lilikuwa na habari 2,3 za juu ya Mbeya City. Binafsi sioni kipya saaana hasa kwa soka la Tanzania! Timu ndogo ni ndogo tu,japo Rafiki yangu Frank Sanga kwenye makala yake ya gazeti la leo Mwanaspoti No.1402 kuna sehemu kaandika hivi "katika mchezo hakuna timu ndogo wala kubwa,ila kuna timu kongwe na timu za kawaida" offcourse ni maoni yake na ni mtu wa soka,ila nahisi vile vile kama Mbeya City hii ingepigwa au kufanywa kama Ashanti,tusiongea hayo yote! Hapo hapo kwenye makala ya Edo Kumwembe "HISIA ZANGU" kaiongelea kwa kina hii hii Mbeya City. Nimewaelewa. Lakini sasa jamani tangu soka la Tanzania liwepo,tokea 1935(Yanga ilianzishwa) na 1936(Simba ilianzishwa),kuna timu zimewahi kuzishusha hadhi timu hzi kiasi cha watu kuzisahau?? Achana na Coastal Union,Maji Maji,Mtibwa Sugar,na nyinginezo kuwahi kubeba taji la Ubingwa. Je,ziko wapi sasa hivi? Nani anaikumbuka Kagera Sugar ya mwaka 2005 kuja mpaka 2010 hv,ilikuwa moto chini,ilimpiga Simba fainali ya Kombe la Tusker,lakini mpaka leo,ni wenzetu wa kutusindikiza katika ligi. Nani haijui Kajumlo Fc? Ikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo,ilikuwa hatari. Lakini leo haipo,hata Moro Utd nayo kwisha habari yao! Timu nyingi zinaanzaga kwa mbwembwe lakini baadae bwana zinapotea,na kuwaachia "wenye ligi". Hata huko Ulaya hakuna tofauti kuuubwa kivile,mnaikumbuka QPR? Ilikuwa ilianza na mbwembwe nyingi,ikamsajili mpaka Brazil One-Julio Cessar lakini wako wapi? Chalii! Sasa hawa Mbeya City,wallahi hata iweje! Hawatamaliza hata kwenye 5 bora! Huo ndo mpira wa Tz bwana. Mpira ambao kabla ya mechi,uwanja unachimbiwa Mayai chini,mpira ambao Viongozi wa TFF ndio mashabiki na wanachama wa "timu kubwa". Hata Azam wanakuja na wanatikisa haswa! Ni kwa sababu pale kuna mpunga wa maana,lakini hata Kajumlo World Soccer chini ya Alex Kajumlo,ilikuwa kama Azam,iko wapi? Tanzania bila #Simba na #Yanga haiwezekani! Hebu fikiria siku moja,bingwa awe hiyo Mbeya City yenu,makamu bingwa awe Mtibwa labda,na mshindi wa tatu awe Azam,kwenye michuano ya kimataifa na ile ya Cecafa ngazi ya vilabu mechi zikiwa zinapigwa hapa Dar. Uwanjani watapata watu wangapi? Hata gharama za maandalizi ya mechi hataweza kulipwa kwa mapato ya tiketi! So,nyie Mbeya City,chonde chonde cheza kwa step,mtaja kupasuka mapafu bure kwa mpira wenu wa jihad wakati mnajua hali halisi ya Soka letu. Wa kuwasifia wawasifie lakini wasivuke mpaka,kana kwamba mnachokifanya hakijawahi kuwepo hapa Tz. Mimi napenda sana jezi zenu! Zinavutia! Ila kwa mpira,chezeni lakini kaa mkijua kufika mbali ni ndoto,hata mfukie Mayai ya Mbuni wa hifadhi ya Tarangire nzima. Tuangalie Mwakani itakuwaje! Siwavunji moyo,wala kuwatia nguvu,nawapa "makavu live". Simba na Yanga zikifa na mpira na utajiri wa soka la bongo umekufa,tumezaliwa tukakuta hivo,tumekua tumekuta hivo,tutakufa tuache hivo hivo! Naipenda Simba Lunyasi,ila sitaki Yanga ipotee mazima,iwepo ili tupate raha ya kwenda kwenye kijiwe cha kahawa kubezana,tupate kununua Mwanaspoti,Dimba,Bingwa,Championi kila siku na kuwaweka mjini Wahariri. La sivyo,hakuna wa kununua Gazeti kwa Habari ya Mbeya City kumsajili Mwafiale wa Tukuyu Starz. Kwa kumalizia,nawashauri hawa Mbeya City wacheze mpira wao,ili waendelee kuwepo ligi kuu,la sivyo mtaifuata Maji Maji,Transit Camp,Kahama United,AFC,n.k. Tanzania Bila Simba na Yanga ni ndoto! Siyo leo,itachukua muda saana tena saana! Simba na Yanga zipo toka mwaka 1936,miaka 77 sasa,hazijawahi kufa wala kushuka daraja! Zipo,achana na ubora wa wao kujijenga ki-miundo mbinu. Ila kwa mpira aisee,sahauni kuzitokomeza. Zitayumbishwa tu,ila kupotea siyo rahisi. NIMEMALIZA... #Sweetbert_Rwabukambara.
Posted on: Tue, 24 Sep 2013 15:34:58 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015