Mr Rwegoshora alimaliza LLB yake hapo Mlimani na kuamua kurudi - TopicsExpress



          

Mr Rwegoshora alimaliza LLB yake hapo Mlimani na kuamua kurudi kwako BKB kusaidia wateja ambao wana matatizo ya kisheria. Siku ya kwanza wakati ndio amefungua ofisi yake,alimuona kijana mtanashati anakuja kuelekea ofisini kwake. Hapo ndipo alipoanza kunyanyua mkono ... wa simu ya TTCL, wakati anajizungusha kwenye viti virefu. Wakati kijana alipokaribia Rwegoshora alionesha kumkaribisha wakati anaongea na simu,alisikika akiongea No.no, no, Absolutely no, You tell those clowns in New York that I wont settle this case for less than one million. (pause) Yes, yes . The Appeals Court has agreed to hear that case next week, Ill be handling the primary argument and the other members of my team will provide support. Okay. Pliz dont forget to tell the State Prosecutor that Ill meet with him next week to discuss the details. Yule kijana ametulia tu anamuangalia bwana Rwegoshora anajinyonganyonga kwamuda zaidi dakika 5. Baada ya kumaliza kuongea na simu,bwana Rwegoshora alielekea kwa huyu jamaa. Samahani sana, kwa kukupotezea muda wako, unajuatena kazi zetu hizi unaumiza kichwa sana, kama unavyoona tena mwenyewe hapa, yaani nikobusy sana, ninapokea simu mpaka nimechoka mwenyewe. enh by the way, what can i do for you? Jamaa alijibu. Mimi ni mfanyakazi wa TTCL, nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani
Posted on: Wed, 30 Oct 2013 13:12:06 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015