Mtanzania anaswa na ‘unga’ Uarabuni WAKATI Waziri wa - TopicsExpress



          

Mtanzania anaswa na ‘unga’ Uarabuni WAKATI Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, akivalia njuga vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kufichua mikakati inayotumiwa na wafanyabiashara kuzivusha kwenye viwanja vya ndege, Mtanzania mwingine amebambwa na dawa hizo mjini Sharjah, Falme za Kiarabu. Hii si mara ya kwanza kwa raia wa Tanzania kukamatwa na dawa hizo nje ya nchi katika mataifa mbalimbali, jambo ambalo limeifanya serikali kuanza kuchukua hatua za makusudi kubaini mtandao huo. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na gazeti la Gulf News la Agosti 19 mwaka huu, Mtanzania huyo ni kati ya watu watano waliokamatwa na dawa hizo huku watatu wakitoka nchini humo na mmoja anatoka visiwa vya Comoro. Ilielezwa kuwa Jumatatu wiki hii, idara ya polisi ya kupambana na mihadarati pamoja na timu nyingine nchini humo iliwakamata watuhumiwa hao kisha kushtakiwa kwa magendo na kumiliki kiasi cha kilo19 za heroin na nne za bangi. Taarifa ya gazeti hilo iliyoandikwa na Jumanna Khamis, ilisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kuliwezeshwa na taarifa za siri kutoka kwa raia wema kuwa kundi hilo lilikuwa na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya. Polisi wa mji wa Sharja kwa kushirikiana na polisi wa Dubai na idara ya kupambana na mihadarati ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Falme za Kiarabu, walifanikiwa kuchunguza kiundani na kubaini mienendo ya watuhumiwa wawili ambao walikuwa na kilo mbili ya bangi na gramu 150 za heroin. Watuhumiwa wengine watatu walikamatwa baada ya kukutwa na dawa za kulevya walizokuwa wamezifuka katika jangwa eneo la Sharjah mjini na Ajman. Kamanda mkuu wa majeshi ya Sharjah, Meja Jenerali Humaid Mohammad Al Hudaidi, alisema kuwa ushirikiano wa timu ya polisi wote katika Falme za Nchi za Kiarabu uko makini kuongoza harakati za kukamata wasambazaji na wauzaji wa dawa za kulevya. Aliongeza kuwa kwa njia ya matumizi ya vifaa bora, mbinu za kimkakati na vyanzo vizuri vya taarifa, polisi wameweza kuwafichua watu hao waliokuwa na lengo la kusambaza na kuuza dawa za kulevya kwa vijana katika nchi za Falme za Kiarabu. #tanzania_daima
Posted on: Sat, 24 Aug 2013 01:29:20 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015