Nasaha za asubuhi No.3 VIPI KUEPUKANA NA KUUKABILI - TopicsExpress



          

Nasaha za asubuhi No.3 VIPI KUEPUKANA NA KUUKABILI MITIHANI: Katika walio kumbwa na mitihani mizito ni Manabii kisha wafuasi wao na walio chini yao katika Imani. Kila unapokumbwa na mitihani basi Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anakupenda. Kwa kuwa mitihani haina budi kumkabili Muislamu, swali muhimu ambalo inafaa sisi tujiulize na tuweze kufahamu ni je tutaikabili vipi mitihani hiyo? Mitihani inaweza kukabiliwa tu kwa njia sahihi alizotufundisha Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Bila ya kufanya hivyo basi tutakuwa tunafanya kazi ya bure. Miongoni mwa maandalizi ni: 1.Kujitahidi katika Ibaadah kama Swalah kwa wakati wake pamoja na kutekeleza nguzo zake, Swawm, Zakah, Hijjah, kumdhukuru Allaah. Mbali na zile Ibaadah za faradhi inafaa pia tujitahidi katika Sunnah za Ibaadah hizo. Mfano funga ya Jumatatu, Alkhamisi na kadhalika, Swalah za Sunnah za qabliyah na baadiyah. Kuhusu Swalah tunapata katika Qur-aan 2: 45, Funga 2: 183. 2.Kusoma Qur-aan kwa kuzingatia maana yake na kufanya juhudi katika kutekeleza amri zake. 3.Kumtii Allaah na Mtume Wake (Qur-aan 4: 13). 4.Kusuburi na kuwa mvumilivu. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu ila kwa wanyenyekevu” (2: 45). 5.Kumtegemea Allaah Aliyetukuka katika mambo yako. Huko ni kuamini kuwa hakuna linaloweza kukukumba isipokuwa kwa idhini ya Allaah Aliyetukuka. Imani hiyo itakufanya usitingishike na lolote hapa duniani. Hakuna anayeweza kukubabaisha. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpatia nasaha Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘Anhu) na hivyo kutupatia sisi pia pale alipomwambia: “…Ukimuomba muombe Allaah; ukitaka msaada taka kwa Allaah. Na ujue ya kwamba hakika lau watu wakusanyike ili wakunufaishe wewe kwa jambo lolote, hawawezi kukunufaisha ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah; na wakikusanyika ili kukudhuru kwa jambo lolote, hawawezi kukudhuru ila kwa jambo Alilokuandikia Allaah. Kalamu zimeinuliwa na kurasa zimekauka…” (at-Tirmidhiy). 6.Kuamini Qadari (mipango) ya Allaah. 7.Imani ya kuwa siku moja utasimama mbele ya Allaah na Atakuhukumu kwa uadilifu. Kwa mema zawadi yako ni Pepo na kwa maovu ni Moto. 8.Kusoma visa vya Mitume na watu wema na mitihani waliyokumbana nao na jinsi walivyoweza kufaulu. Inaendelea....
Posted on: Fri, 04 Oct 2013 05:30:08 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015