Ni fursa adimu na adhimu mpenzi wa NURU YA LUGHA 102.7(NAIROBI) - TopicsExpress



          

Ni fursa adimu na adhimu mpenzi wa NURU YA LUGHA 102.7(NAIROBI) RADIO MAISHA, wadhamini wetu ni Shirika la Uchapishaji Vitabu la LONGHORN. Nahodha wa kipindi Jumamosi hii ni mimi Malenga wa Mlima Elgon, Geoffrey Mung’ou. Makinika ili ujishindie Kiswahili Mufti, Kamusi ya Wanafunzi Kiswahili-Kiingereza, Kamusi ya Karne ya 21, Kamusi Kibindo miongoni mwa kamusi nyingine. Aidha tunavyo vitabu kuntu vya hadithi(ambavyo ni vipya)-Siri Sirini, Mkamandume, Mbali na Nyumbani, Janga la Werevu, Kimya, Kimya, Kimya, Gharama ya Amani na vitabu vingine vingi. MASWALI YATAKUWA MBOGA CHAMBILECHO.... Kazi kwako. Mti uitwao mchikichi huitwaje katika Kiingereza? Gali la kijani nimenunuliwa. Eleza matumizi ya la.
Posted on: Sat, 09 Nov 2013 05:39:36 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015