RIYADH: Saudi Arabia imeikataa nafasi ya kuwa mwanachama wa - TopicsExpress



          

RIYADH: Saudi Arabia imeikataa nafasi ya kuwa mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikisema baraza hilo lenye wanachama 15 halina uwezo wa kusuluhisha migogoro duniani. Hatua hiyo imefuatia baada ya kuchaguliwa kwa nchi hiyo kuwa miongoni mwa wanachama 10 wasio wa kudumu katika baraza hilo. Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Saudi Arabia na kuripotiwa na vyombo vya habari nchini humo, imesema Baraza la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutekeleza majukumu yake kuhusu Syria. Imesema kushindwa huko kuliipa serikali ya rais Bashar al-Assad uwezo wa kuuwa watu wake, hata kwa kutumia silaha za sumu bila kuchukuliwa hatua zozote. Saudi Arabia imesema pia katika taarifa hiyo, kuwa Baraza la Usalama limeshindwa kuutatua mgogoro wa Israel na wapalestina, na halikuweza kuifanya Mashariki ya Kati eneo lisilo na silaha za maangamizi.
Posted on: Sat, 19 Oct 2013 07:16:38 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015