Rais Uhuru Kenyatta awaandalia Waislamu futari Ikulu Nairobi - TopicsExpress



          

Rais Uhuru Kenyatta awaandalia Waislamu futari Ikulu Nairobi Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewaandalia Waislamu futari katika Ikulu ya Rais mjini Nairobi ambapo amesisitiza kuwa serikali yake inataka kuwaunganisha Wakenya wote. Akihutubu katika dhifa hiyo ya futari iliyohudhuriwa na mamia ya Waislamu wa matabaka mbali mbali Jumamosi usiku, Kenyatta alisema hatua yake ya kuwaalika Waislamu kufuturu Ikulu ni njia ya kuonyesha kufungamana kwake na Waislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Posted on: Sun, 21 Jul 2013 03:52:14 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015