Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, tuhuma za utumiwaji - TopicsExpress



          

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, tuhuma za utumiwaji silaha za kemikali zinazoelekezwa kwa serikali ya Syria, ni upuuzi mtupu. Putin amesema kuwa, kile kinachotakiwa kwa Washington ni kuleta ushahihdi wa wazi mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unaothibitisha madai hayo ya silaha za kemikali nchini Syria na kusisitiza kuwa, ikiwa Marekani itajichukulia hatua peke yake ya kufanya mshambulizi dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu, kwa hakika litakuwa suala baya kabisa. Aidha rais huyo wa Russia amemhutubu rais wa Marekani kwa kusema kuwa, Obama ambaye ametunukiwa tuzo ya amani ya Nobeli, anatakiwa kufikiria mara mbili juu ya mashambulizi ya Marekani, yatakayowalenga raia wasio na hatia huko Syria, ikiwa uvamizi huo utatimia. Wakati huo huo Yuri Ushakov, Mshauri wa rais huyo wa Russia katika masuala ya nje amewambia waandishi wa habari kuwa, hakuna nchi wala muungano wowote wa nchi wenye haki ya kuishambulia nchi nyingine bila ushahidi wa kutosha. Amesema kuwa, ikiwa mashambulizi ya upande mmoja yatatekelezwa dhidi ya Syria, basi hilo litakuwa pigo kwa Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.
Posted on: Sun, 01 Sep 2013 09:31:03 +0000

Trending Topics



Recently Viewed Topics




© 2015