Ramadhan Shiraz Chelsea, Christian Simba, Deogratius Laizer HEBU - TopicsExpress



          

Ramadhan Shiraz Chelsea, Christian Simba, Deogratius Laizer HEBU SOMENI HAPA! Baada ya sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange,producer Shedy ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuuanika ukweli wa mambo.... Akiongea na #Team tizniz,Shedy amefunguka kama ifuatavyo: “Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu. "Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midumdo niliyonayo. "Bila hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali kama mteja, ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo. "Baada ya Diamond kuupenda mdundo huo, niliamua kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa, "Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali yeye mwenyewe."
Posted on: Thu, 05 Sep 2013 20:30:34 +0000

Recently Viewed Topics




© 2015